Swali: Wachezaji wetu wakienda kucheza kimataifa huwa wanalipwaje

Nilisikia wiki iliyopita sijui radio gani walikuwa wanazungumzia maswala ya hamasa kwamba jamaa kuna malipo ya karibuni kama mara 2 hawajalipwa lakini utashangaa kamati ya hamasa wanalipwa.
 
Serikali Wala tff hawajawahi kuwalipa wachezaji wa timu ya Taifa!. Wachezaji wanajitoa Kama vijana wanaojiunga jkt.
 
Inafaa walipwe, ila sina uhakika kama wanalipwa.
 
Najua kuwa wanalipwa posho
Anayejua anirekebishe
 
Je ni mshahara au per diem. Na je malipo ni flat rate au?

Ama ndio mambo ya uzalendo kujitolea?
Kuna per diem lazima wapewe kwa kila siku wanayokua kwenye mtoko wa mechi so wanaweza lipwa kama lumpsum wakimaliza mizunguko yote. Bajeti inakuwepo TFF so serikali inatiririsha hela huko kwa ajili ya mambo kama hayo na zingine zinachangishwa na wadau wa michezo, sponsors wa timu ya taifa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…