Swali, Youtube huwa wanalipa kutokana na nchi uliosajili chaneli yako?

Hata watanzania unaweza kuwa tajiri kupitia youtube . Mchawi content za kuvutia watu tu. Hukosi dollar 5000$-50,000$ kwa mwezi
Ebu tupe elimu, inakuwaje kuwaje kuipata hiyo $ 5000? Na watazamaji wanatakiwa watokee wapi.
 
Kuna sehemu nilisoma andiko, likisema Youtube za Canada, USA, UK ndio wanalipwa vizuri, sababu ya msingi sikuweza kuipata.​
Sababu ya msingi ni moja tu matangazo yanayoonekana kwenye hizo video kampuni zinapata faida (ROI ) kubwa kuliko yakionekana kwa wabongo. Mfano betway katangaza tangazo lake mbongo akaona akajiunga akabeti jero😂 tangazo hilo hilo Mtu wa USA akaliona akajiunga akabeti $100,000 wewe huoni tofauti ? Yupi atakuwa amefaidisha kampuni? Kwenye matangazo dunia imegawanywa kwa Tier, kuna Tier 1, Tier 2 na Tier 3 tanzania ipo kwenye 3 hao usa, canada , uk, na nchi nyingi za ulaya zipo Tier 1 , africa ni tier 3 nako kuna makundi mfano Tanzania sio sawa na southafrica, wapo juu yetu. sasa hapo kuna kitu kinaitwa CPM , cost per thousands impression . Adverser atalipa ngapi kwa kila watu walioona tangazo 1000? Utakuta tier 1 wanalipa CPM kubwa ukilinganisha na CPM ya Tanzania ambayo ni 0.03CPM kwa kila views 1000
 
Ukiwa na hiyo 10M views kwa mwezi then wakawa wanalipa 1$ kwa kila 1000 views una 10000$ sasa hapo itategemea na niche yako pia na visitor unawapokea kutoka wapi
Kupata hiyo view 10m naona ni ndoto, ata hizo video nilizo ziambatanisha hazina hizo view.
 
Wanalipa kutokana na nani kaangalia.

Mfano mtu ka upload video Wamarekani 1000 Waka angalia, mwengine ka upload video watanzania 10,000 Waka angalia, yule mwenye 1000 wa Marekani watapata hela zaidi.

Ukiwa publisher huwa rate unaziona.
YouTube analipa watengeneza maudhui kwasababu na yeye kalipwa na wafabyabishara kuleta matangazo kwake, watazamaji tunatakiwa si kuona tu tangazo ni pamoja na kununua bidhaa au huduma.

Sasa watazamaji wa nchi zetu hatina utamaduni wa kununua vitu mtandaoni, pila nguvu yetu ya kipato ni ndogo, kwahiyo malipo kwa mtengeneza maudhui wa nchi zetu ni ndogo, na wa nje ni kubwa.
 
Binafsi mm nina YouTube channel yenye subscribers zaidi ya 16K. Na subscribers wangu 50% ni south africa, 30% ni USA, 15% ni wakenya na waliobaki ni watu wa nchi mbalimbali afrika. Vigezo takribani vyote vimetiki isipokuwa kimoja tu, ishu ya ku-own content zangu mwenyewe. Yaani hapo tu.
 
Kupata hiyo view 10m naona ni ndoto, ata hizo video nilizo ziambatanisha hazina hizo view.
Sio ndoto mkuu watu wengi sana wanapata hizo views 10M kwa mwezi kwa bongo. Hizo video zilizoambatanishwa kwa haraka haraka hao hawakosi 100,000$ kwa mwezi. Mtu una video 100 kila video ipate views 200k kwa mwezi unadhani ni views wangapi? Afu kuna watu wana video mpaka 5000 na kuendelea
 
Sasa kama hauna content niuongo mkuu huwezi kutoboa
 
Ni vizuri wewe upo field unaweza kutupa majibu sahihi, Kwa status uliopo, imeshaanza kukuingizia mapato, na je yanaridhisha?​
 
lakini view zao ni chini 10m ndani ya mwaka mzima
 
Asante kwa ufafanuzi mkuu. Je, mtu anaanza kulipwa anapofikisha viewers wangapi na rates zikoje mkuu?
 
Hivi hata hizo bongo series zinapitia mgongo ule ule. Kwa sasa kuna watengeneza films wengi wanaweka series zao YouTube na ukiangalia mahadhi yake unaona kuna investment imetumika kutengeneza. Je inawalipaje?...

Nakumbuka inasemekana urefu wa video unachangia, mfano video ya dakika tatu na film ya dakika 30.. Filamu zinapokea zaidi per view

Lakini pia hata quality ya video na content yake..

Je vigezo hivi vipo sahihi na kama kuna vingine ni vipi mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…