Swali

4X4byfar

JF-Expert Member
Joined
Oct 29, 2008
Posts
201
Reaction score
21
Ni mambo gani ya kujiepusha nayo mwanamke kumtendea mwanamme asijekumuacha. Bora kinga kuliko dawa...naombeni ushauri tafadhali.
 
Sheria ya dhahabu au Golden Rule inafaa sana kujibu swali lako.

Mtendee mwenzako unayotaka utendewe, na usimtendee mwenzako usiyotaka utendewe.
 
Sheria ya dhahabu au Golden Rule inafaa sana kujibu swali lako.

Mtendee mwenzako unayotaka utendewe, na usimtendee mwenzako usiyotaka utendewe.

Nimekupata asante...je unakuta yeye anakutenda usiyopenda kutendwa, ni mtende vipi hapa!
 
Usimnyime chakula cha ndoa...

Asante je kama matendo yake yamenipelekea kumnyima chakula cha ndoa! kila ukimshauri anitende hivi ndo napata ashki then hafanyi bado mtu utakosa kumyima kwa kuwa mimi ni kisiki cha mpingu au?
 
Ngoja Fidel and Co waje hapa nadhani watakuwa na mchango zaidi....
 
Je yeye anajua kua UNAMPENDA?
Kumpenda bila kumwonyesha UNAMPENDA haisaidii.
Wanawake wanapenda KUPENDWA hivyo mwonyeshe wampenda ataKUPENDA pia.
 
mapenzi hayana formula bwana...yana flo tu yenyewe palipo na penzi la kweli! wewe kula kuku usiwaze mambo ya kuwachwa sijui nini, kama wa kukuacha atakuacha tu hata ukimfungia novena.
 
Je yeye anajua kua UNAMPENDA?
Kumpenda bila kumwonyesha UNAMPENDA haisaidii.
Wanawake wanapenda KUPENDWA hivyo mwonyeshe wampenda ataKUPENDA pia.


Pengine kukujibu tuu kuambatana na vipengele vyako ndugu yangu;-
- Natumaini analifamu hilo nampenda maana ni jambo naliongea sana kila siku.
- Kumuonyesha kuwa nampenda na fanya hivyo sana pengine ungenipa usaidizi zaidi ni mambo gani mwaumme huona kuwa kapendwa na mwanamke!
- Nikweli tunapenda kupendwa na sisi pia tupendwe jamani. Maana unajikuta wewe unatoa tuu kupokea zero, zaidi unaanza kujihisi kama toy vile!
 
Ushauri wangu 4 x 4 ni kwamba kwanza jipende wewe mwenyewe.kwa kula vizuri, kuvaa vizuri, kuwa mkarimu , timiza wajibu wako kwa mume na watoto kama wapo. Mengine ni magumu sana kuyabadilisha. Wanawake pia huwa tunafikiria mambo mengi kwa wakati mmoja, punguza kuulizia issues au kuongelea matatizo( kulalamika). Try ti make yourself happy by all means. hapo kwa kweli mwanaume ataona mwanamke si ndio huyu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…