FaizaFoxy
Platinum Member
- Apr 13, 2011
- 100,246
- 123,145
Swanglish ni Kiswahili na Kingereza vinapooanishwa vikipenda visipende.
Si ajabu kukumbana na maandiko au maongezi ambayo wengi wetu hujikuta tunaoanisha Kiswahili na Kingereza bila kudhamiria.
Jee, ni wangapi wanafahamu maneno ya Kingereza tunayo wapachikia katika Kiswahili? Ukichukulia kuwa huwa tuna bofya "bombastic" ambazo hata kwa anaeelewa Kingereza lazima akajikumbushe kwenye "dictionary."
Jee, ni wangapi ambao hupachika tu maneno ya Kingereza bila hata kuoana na sentensi wanayoiongea/andika? Hawa huwa hawaelewi na wanapachika tu neno lolote linalowajia iki waonekane wanaelewa au huwa neno hilo wanalielewa kivingine?
Umekumbana na lipi likakufanya ucheke, japo kimoyomoyo? Au umekutana na lipi likakufanya usielewe kabisa ulichoambiwa lakini ukakubali tu mradi yaishe?
Ni sahihi kutumia Swanglish?