SI KWELI Sweden imeanzisha mashindano ya ngono kama mchezo

SI KWELI Sweden imeanzisha mashindano ya ngono kama mchezo

Baada ya kuitathmini taarifa hii, tumebaini kuwa si ya kweli.
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Sweden imepitisha ngono kama sehemu ya Michezo na itaandaa na kuwa mwenyeji wa Mashindano ya kusimamia kucha Huku Ulaya.

1686307032100.png
 
Tunachokijua
Hivi karibuni kunako mitandao mingi ya kijamii imeenea habari ikidai kwamba nchi ya Uswidi (Sweden) imekubali kuitambua ngono kama sehemu ya mchezo na inaandaa mashindano ya mchezo huo hivi karibuni.

Kichwa cha habari kwenye tovuti ya The Times of India, moja ya magazeti mashuri nchini India lilichapisha habari iliyokuwa na kichwa kilisema "Hivi karibuni Uswidi Itakuwa Mwenyeji wa Mashindano ya Ngono ya bara la Ulaya". Taarifa hizo zinadai kwamba mashindano haya yalikuwa yamepangwa kuanza tarehe 8 Juni katika mji wa Gothenburg nchini humo. Habari hiyo pia ilikamata vichwa habari vya mataifa mbalibali ikiwamo Pakistan, Nigeria na Ugiriki.

Zaidi ya taarifa hiyo kuchapishwa na kusambaa kwenye mataifa mbalimbali pia uvumi huu umeenea katika kurasa mbalimbali za mitandao ya kijamii ya nchini Tanzania ikiwamo JamiiForums na vyombo vingine vya bahari vya Afrika Mashariki.

Je kuna uhalisia kuhusu kuwapo kwa shindano hili?
JamiiForums imepitia vyanzo mbalimbali ili kujua uhalisia wa jambo hili ambao imepata taarifa zifuatazo.

Kwa mujibu wa Anna Setzman, Msemaji Mkuu wa Shirikisho la Michezo la Uswidi, amekanusha nchi yake kuanzisha Shindano hilo.

Anna anasema:

"Habari zote zinazosambaa kuhusu nchi yetu kutangaza ngono kama mchezo na kuandaa mashindano ni uongo".

Je uvumi huo ulianzaje?
DW wanafafanua kuwa uvumi huo kuhusu Uswidi ulisababishwa na mtu mmoja raia wa Uswidi aliyeitwa Dragan Bratic ambaye anamiliki Vilabu vya Wanawake kucheza uchi usiku (Strip Club). Inaelezwa kuwa Bratic hivi karibuni alituma maombi kwa Shirikisho la Michezo la Usiwdi akitaka ngono itambulike kuwa miongoni mwa michezo kama michezo mingine nchini humo na Shirikisho hilo likakataa.

Baada ya tukio hilo Shirikisho hilo lilitoa taarifa hiyo ya kukataa ombi la Bratic. Hivyo, tatizo likaanzia kwenye baadhi ya vyombo vya habari vilivyoripoti taarifa hiyo.

Kwa ufupi, madai ya Uswidi (Sweden) kutangaza ngono kama mchezo na kuandaa mashindano ni uongo, na Shirikisho la Michezo la Sweden limekana kuhusika au kutambua Mashindano hayo.

Hivyo, kutokana na vyanzo vilivyopitiwa na JamiiForums inaona kwamba uvumi wote kuhusu Uswidi kuitambua ngono kama mchezo ni uzushi.
Back
Top Bottom