BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,591
- 8,826
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. @mwigulunchemba (Mb) amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Sweden nchini Tanzania, Mhe. Charlotta Ozaki Macias, ambaye ameahidi kuwa nchi yake itashiriki kugharamia ujenzi wa reli ya kisasa ya SGR kipande cha tatu kinachoanzia Makutupora mkoani Singida hadi Tabora na kipande cha nne kinachoanzia Tabora hadi Isaka.
Katika mazungumzo yao Mhe. Nchemba ameishukuru Sweden kwa kushiriki kikamilifu katika maendeleo ya Tanzania, ikiwemo kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) Lot 2, kipande kinachoanzia Morogoro hadi Makutupora mkoani Singida, ambacho ujenzi wake umekamilika kwa asilimia 96 na kwa utayari wa nchi hiyo kutoa fedha kwa ajili ya kujenga reli kipande cha tatu kinachoanzia Makutupora mkoani Singida hadi Tabora na kipande cha nne kinachoanzia Tabora hadi Isaka.
Soma pia: Uzi mkuu unaoonesha yaliyojiri kwenye mradi wa SGR tangu kuanza kwake mpaka mradi ulipofikia hivi sasa
Ziara ya Balozi huyo wa Sweden Mhe. Charlotta Ozaki Macias, aliyeambatana na Balozi wa Biashara Endelevu kutoka Wizara ya Mambo ya Nje ya Sweden, Bi. Cecilia Ekholm, ni ufuatiliaji wa matokeo ya ziara ambayo Mhe. Dkt. Nchemba, aliongoza ujumbe wa Tanzania katika nchi za Scandinavia, ikiwemo Sweden, mwezi Septemba, 2023