Swine Flu in Africa - Tahadhari!

Mkazi wa Bagamoyo mkoa wa Pwani, amelazwa hospitali ya Taifa ya Muhimbili akifanyiwa uchunguzi baada ya kuonekana akiwa na dalili za ugonjwa wa homa ya mafua ya nguruwe.
Akizungumza na Nipashe jana jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma za Kliniki hospitalini hapo, Profesa Andrew Swai, alisema walimpokea mgonjwa huyo lakini bado madaktari wanaendelea kumfanyia vipimo ili kubaini kama anaumwa ugonjwa huo au la.
Profesa Swai alikataa kumtaja jina mtu huyo na lini walimpokea kwa madai kuwa, bado hawajahakikisha kama kweli anaumwa ugonjwa huo au ni mafua ya kawaida.
Toka ugonjwa huo utangazwe hapa nchini mapema mwaka huu, jumla ya wagonjwa watatu wakiwemo ndugu wa tumbo moja, raia wa nchini Uingereza wamelazwa hospitalini hapo baada ya kubainika kuwa na virusi vya ugonjwa huo (H1N1) walipowasili uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere.
 
patakuwa hapatoshi mjini hapa!mungu tuondolee hili balaa
 
Tatizo ni waandishi wetu ambao wanashindwa kujua ni habari zipi za kuzipa kipau mbele,yaani wanashindwa kabisa kufahamu kuwa jambo bado halijathibitishwa na madaktari wao wamevamia ,sasa hawaoni kama wanaiingiza nchi nzima na raia zake katika matatizo na inawezekana kabisa ikawekwa kwenye black list ,hao waingereza mbona huko kwao wamebana kimya hawajawaanika ? Mijitu mingine nuksi ile mbaya ?
 
ni bora watangaze sishangai ni waingereza ndio waliobainika bora watu wajiadhari especially kipindi hiki cha likizo ambacho watoto wengi na familia nyingi zipo huko holiday ila nimefurahi kama wanacheki watu airport, uk ipo kimya wpte wapo huko sasa.
 
10th July 2009

Nguruwe.

Taarifa zilizopatikana jana kupitia vyombo vya habari, zimeonyesha kwamba tayari ugonjwa wa mafua ya nguruwe unaosababishwa na virusi vya H1N1 umeingia Tanzania.

Hii ni kutokana na kuwepo kwa mgonjwa wa mafua hayo katika Hospitali ya Taifa Muhimbili ambaye ni mwanafunzi kutoka Uingereza aliyewasili nchini Julai 4 kupitia Kenya kwa Shirika la Ndege la Kenya.

Imeelezwa kwamba mwanafunzi huyo ni miongoni mwa wanafunzi wengine 15 pamoja na waalimu wanne waliokuja Tanzania kwa ziara ya kufanya kazi nchini kwa kujitolea.

Kwa tukio hilo, sasa ardhi ya nchi tatu majirani; Tanzania, Kenya na Uganda inao wagonjwa wa mafua ya nguruwe, ugonjwa ambao ulianzia nchini Mexico mwezi Aprili mwaka huu kabla ya kusambaa katika nchi nyingine duniani, hususan Marekani na Canada.

Uwepo wa ugonjwa huu katika nchi hizi za Afrika Mashariki ni suala linalofanana kwani mgonjwa wa Kenya alitokana na wanafunzi wa Uingereza waliokuwa nchini humo hivi karibuni, halikadhalika mgonjwa wa Uganda naye alitokea Uingereza kupitia Kenya.

Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO), ugonjwa huo umeshasambaa kwa nchi zaidi ya 100, ambapo watu zaidi ya 71,000 wameugua huku takriban 310 wakifariki dunia.

Mwanzoni mwa mwezi huu, mkuu wa WHO, Dk. Margaret Chan, alionya kwamba ni vigumu kudhibiti ugonjwa huo usisambae zaidi, hivyo akasisitiza katika tiba na kupambana nao.

Wizara yetu ya Afya jana ilitoa taarifa kwa umma kwamba hakuna maambukizi mengine mapya nchini na kwamba itakuwa inawafuatilia kwa karibu wanafunzi wa Uingereza waliobaki pamoja na walimu wao baada ya kuwapima na kuonekana hawana dalili za ugonjwa huo.

Haikufafanuliwa vyema huko kufuatiliwa kwa karibu ni kwa aina gani, lakini wenzetu nchini Kenya, wanafunzi wa Uingereza waliwekwa kwenye kizuizi maalum kwa siku kadhaa wakichunguzwa.

Nchini Ufilipino, watu wanaotokea katika nchi zenye wagonjwa wengi hutakiwa kubaki majumbani mwao ama mahotelini walikofikia kwa uangalizi maalum wa maofisa wa afya kwa siku takriban 10.

Kwa sasa mgonjwa wetu ameingia nchini kwa njia ya ndege, lakini kwa vile tayari ugonjwa huu umepiga hodi pia nchini Zimbabwe, bila shaka muda si mrefu tutaanza kupata wagonjwa wengi zaidi wakiwemo wale wanaoingia nchini mwetu kupitia kwenye mipaka na njia za panya.

Tunadhani si wakati wa kuzubaa na kusikilizia kama kuna mgonjwa mwingine na kutoa matangazo haya na yale isipokuwa ni kuanza mkakati mahususi kwa vitendo katika kupambana na ugonjwa huu ambao umeshaua watu zaidi 300 duniani kote ili kuudhibiti.

Tunaisisitiza serikali, kama ilivyoahidi, kuimarisha utaoji wa mafunzo kwa wafanyakazi wa afya na jinsi ya kutibu na kuzuia ugonjwa.

Nchini Kenya, inaonekana maofisa wa afya hawakuwa wameandaliwa vyema kwani kulijitokeza malalamiko ya wauguzi kumkimbia mgonjwa aliyedhaniwa kwamba anaweza kuwa na maambukizi ya ugonjwa huo. Tunatazamia hilo halitotokea hapa kwetu.

Serikali pia imeahidi kutoa elimu ya afya kwa umma kupitia vyombo mbalimbali vya habari. Hilo tunaomba lifanyike haraka, ikiwezekana kuanzia leo kutokana na umuhimu wake.

Tunaamini kwamba elimu hiyo pia itataja makundi ambayo yana hatari zaidi yakipata ugonjwa huu ambayo ni pamoja na watoto chini ya miaka mitano, wenye zaidi ya umri wa miaka 65, wajawazito, wenye magonjwa ya moyo, mapafu, na kadhalika.

Sambamba na hilo, tunaweza kuwaiga Waingereza na hata majirani zetu Uganda ambako maofisa wa afya wametoa hadi namba zao za simu kwenye vyombo vya habari ili mtu mwenye dalili za ugonjwa huu aweze kupiga na kupata ushauri wa haraka. Inaelezwa kwamba kwa baadhi ya makundi yenye hatari zaidi yanapopata mafua haya, huhitaji matibabu haraka ndani ya masaa 48 toka kusikia dalili.

Pia tunaweza kuiga kampeni aliyoanzisha Rais wa Ufilipino, Gloria Arroyo, ya kila anayerejea nchini humo kutoka nchi inayoaminika kuwa na wagonjwa wengi wa ugonjwa huu kwenda mwenyewe hospitali ya karibu kupima, hata kama hana dalili yoyote na kujifungia kwake kwa muda akijisikilizia.

Shime, si muda wa kuzubaa. Ni kila mtu kwa wakati wake kupambana ili kuudhibiti ugonjwa huu usije ukatuletea maafa.

CHANZO: NIPASHE
 
Wajinga ndio waliwao,swineflue is a hoax!

 
Tanzania tunatumia njia zisizokuwa na tija kabisa katika kudhibiti usambaaji wa virusi vya H1N1; hebu ona hapa chini. Itabidi tujiandae kufyekwa sana na virusi hivi vya H1N1 vikiingia nchini kama tulivyofyekwa na virusi vya HIV.

Health officials collect forms filled by arriving passengers at the Julius Nyerere International Airport in Dar es Salaam on Sunday. All arriving passengers are required to answer questions about their health status as a precautionary measure against the spread of the deadly new swine flu virus.
 

Mwl Kichuguu

what are your suggestions?
 

Kichuguu!

Wewe huna kazi ya kufanya nini? Tangu hii homa wadosi wanayoita ni ya nguruwe ambayo haijawahi kumpata hata nguruwe mmoja inakuhusu nini.

Tangu ianzishwe huko Mexico na USA sijasikia kuna mtu mwenye ngozi kama yako ameadhirika why worry !! Sisi tuendelee kupambana na njaa na malaria mambo yanayowezekana kuyaondoa tukiwa na dhamira yanayoua akina mama na watoto kwa kwenda mbele!
Hii HINI saizi ya wadosi tuwachie watimue vumbi!! Hao wanaovaa viziba midomo hapo Airoort ya Nyrere bora wangerudi mjini kuchimba mitaro na kuangamiza mazalia ya mbu kalakabaho!!
 

Hebu tupe takwimu ni weusi wangapi wameugua H1N1 tangu ugonjwa uanze? Sisi walitutengenezea HIV sasa acha nao wapungue kidogo
 
Mkuu sasa kwa mwislamu ambaye kwake Swine ni haramu, akipata swine flu itakuwaje?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…