SYMPLE ANALYSIS, masomo ya sayansi ni magumu sana kulinganisha na Arts. WALIMU WA SAYANSI WAWE LULU

Mshinga

JF-Expert Member
Joined
Feb 5, 2013
Posts
3,532
Reaction score
1,126
nisieleweke vibaya na wala sibezi watu waliochukua masomo ya arts ila inapaswa kutoa msukumo mkubwa kwa masomo ya sayansi kama tunataka kuendelea kwenye fani ya sayansi.

MWISHO WA HOJA YANGU NITATAKA MISHAHARA YA WALIMU WA SAYANSI IPEWE KIPAUMBELE ZAIDI NA IWE MIKUBWA TOFAUTI NA MISHARA YA WALIMU WENGINE ILI KUTOA MOTISHA KWA WALIMU adimu wa sayansi.

VIFAA VYA SAYANSI PIA VINATAKIWA KUPEWA KIPAUMBELE KIKUBWA NA IKIBIDI KWA KUANZIA KILA SHULE IWE NA ANGALAU NYUMBA YA WALIMU WA SAYANSI ILI KUWAVUTIA.

pamoja na kwamba mimi si mchumi lakini najua demand increases price, why not walimu wa sayansi wasipewe mishahara mikubwa?

KWA O LEVEL.
1.wanafunzi wengi kidato cha kwanza wanapoanza shule wengi ukiwahoji utabaini wanapendelea masomo ya sayansi ama fani za sayansi kama ndoto zao. hali inaendelea hivi mpaka kidato cha pili ambapo wengine wanaanza kupata shida kuyamudu masomo ya sayansi kiasi cha wengine kukata tamaa na kuamua kuachana nayo mapema. mpaka kufikia kidato cha tatu wengi wanakuwa wameachana na ndoto zao za kusomea fani za sayansi.
TUNAPASWA KUJIFUNZA KITU HAPA NA TUJARIBU KUWA NA JITIHADA KUBWA KULINDA NDOTO ZA WATOTO HAWA KWA KUWAWEZESHA KUYAMUDU VYEMA MASOMO YA SAYANSI MAPEMA.

2.ugumu unaojitokeza katikati ya safari unawafanya wanafunzi wengi kukimbilia masomo ya arts na wanayamudu vyema kwa kiasi kikubwa katika mazingira yaleyale.

HAPA PIA TUNAPASWA KUJIFUNZA KUWA MASOMO YA SAYANSI NI MAGUMU SANA KULINGANISHA NA ARTS HIVYO NGUVU ZINAZOTAKIWA KUIMARISHA UFAULU WA SAYANSI ZINAPASWA KUWA MARA MBILI ZAIDI YA NGUVU ZINAZOTUMIKA KUIMARISHA ELIMU KWA UJUMLA WAKE.

3.matokeo ya kidato cha nne pia yanatoa picha halisi. kwa takwimu za kila mwaka masomo ya sayansi ukiondoa yale ya lazima yanaonekana kuchukuliwa na wanafunzi wachache zaidi ambapo bado matokeo yao yanakuwa mabaya zaidi kuliko ya masomo ya arts kwa ujumla wa matokeo yote.

kwa matokeo ya mtu mmoja mmoja, wanafunzi wengi waliochukua masomo ya sayansi na kufaulu mtihani wa kidato cha nne huwa wamefaulu pia masomo ya arts kwa kiwango pengine cha juu kuliko wanafunzi waliojikita kusoma arts pekee ambao wengi wao huwa hawajafaulu masomo ya sayansi ya lazima kama biology. hapa akili yangu inaniambia kuwa wanafunzi wanasoma sayansi wanaweka nguvu kubwa kwenye masomo ya sayansi na kutoa muda kidogo sana kwa masomo ya arts lakini bado wanafaulu.
HUU NI USHAHIDI MWINGINE WA UGUMU WA SAYANSI NA HIVYO JITIHADA ZA KUIMARISHA SAYANSI ZINAHITAJI KUWA KUBWA ZAIDI.

4.walimu wa sayansi pia ni baadhi tu wanaonekana kuyamudu vyema masomo ya sayansi, na hapa nimeshuhudia walimu wanayoyamudu vyema masomo ya sayansi wakigeuka LULU kwa kufundisha shule nyingi na wakati mwingine wanakuwa maarufu katika eneo kubwa zaidi. lakini hili ni nadra sana kwa walimu wa arts ambao wengi wanayamudu vyema masomo yao na si rahisi mwalimu wa arts kuwa LULU sawa na wa sayansi.

HII TOFAUTI INANIAMBIA KUWA TUNAPASWA SASA KUWACHUJA VYEMA HAWA WALIMU WA SAYANSI WAKATI WA KUWAAJILI ILI TUPATE WALE WENYE UWEZO MKUBWA WA KUFUNDISHA NA KUELEWEKA VYEMA NA HIVYO ITABIDI WAPEWE MISHARA MINONO KAMA TUNATAKA KUIMARISHA SAYANSI ILI WAJIONE WANAJALIWA NA WASIKIMBILIE FANI ZINGINE KUAJILIWA ILI KILA MWENYE UWEZO WA KUFUNDISHA ABAKI KUFUNDISHA NA TUWAVUTIE WENGINE WASIOFUNDISHA WAKIMBILIE UALIMU.

PIA GHARAMA ZA KUSOMA MASOMO YA SAYANSI ZIMEONEKANA KUWA NI KUBWA KULIKO GHARAMA ZA ARTS.

lazima mwalimu wa sayansi awe LULU na baada ya muda nina uhakika tutakuwa tumeimarisha sayansi kwa kupata walimu bora wa sayansi kuliko ilivyo sasa ambapo kila aliyesoma ualimu wa sayansi anaweza kuwa mwalimu wa kuajiliwa serikalini bila kujali kama ana uwezo wa kufundisha ama laa na tunakuwa na lundo la walimu wa sayansi wasiokuwa msaada kwa watoto wanahitaji walimu bora ili kuyaelewa vyema masomo yanayoonekana ni tatizo kueleweka. NIPO TAYARI KWA CHALLENGE HAPA.na kwa hoja hii walimu wengi hata walioacha ualimu watarudi kufundisha na kuacha kazi huko kwingineko waliko.

5.Kuna kitu kingine japo ni kidogo lakini yapasa nikieleze.
nimeshuhudia wanafunzi wanasoma TUITION masomo ya sayansi. unakuta mwanafunzi kaisoma topiki moja kwa walimu zaidi ya wawili kwa sababu wengi wa walimu hawamudu sawa sawa hayo masomo.
HOJA INAONGEZA NGUVU KWENYE HOJA YA HAPO JUU.

ADVANCE LEVEL EDUCATION.
1. wengi wa wanafunzi wanaofaulu kwa kiwango cha division one na two huchukua masomo ya sayansi lakini ni ajabu kuwa hawa hawa waliopata matokeo mazuri ndio watakuja kupata matokeo hafifu form six wakati ambapo wanafunzi wengi wengi wanaochukua masomo ya arts huwa wanapata matokeo mazuri sana form six na kufeli kwao ni jambo la nadra sana pamoja na ubovu wote wa mazingira ya kujifunza na kujifunzia.

hapa natambua matatizo lukuki ya shule zetu za serikali kama chanzo cha ufaulu hafifu ama mbovu lakini hayo niyaweke kapuni kwanza.


KWA HIYO HAPA WENGI WANAOCHUKUA SAYANSI WANAPENYA KWA TAABU SANA ADVANCE KULIKO WA ARTS AMBAO HUFAULU KWA KIWANGO KIKUBWA NA BILA TABU. team sayansi wanajua ninaposema haya.

kwa hiyo KWA VYOVYOTE VILE TUNAHITAJI WALIMU BORA WA SAYANSI WATAKAOLIPWA MISHAHARA SAWA NA SEKTA ZINGINE NYETI KABISA NA MAZINGIRA YAO YABORESHWE ZAIDI.


kama serikali iliweza kuwavutia wanafunzi wa sayansi kwa kuwapa upendeleo fulani kwenye mikopo inawezekana pia hawa walimu wa sayansi wakapewa upendeleo fulani kwenye mishara yao na posho. na waruhusu hata wengine wenye uwezo wa kufundisha hata kama si walimu kitaaluma ili wakaokoe sayansi yetu baada ya kufaulu vyema interview ama utaratibu utakowapa mamlaka wanafunzi wenyewe kukubali kuwa huyu anaeleweka na hivyo apewe ajira baada ya kufundisha kwa muda maalumu.


NIISHIE HAPA KWA KUTOA HITIMISHO KUWA UGUMU WA MASOMO YA SAYANSI USUKUME HOJA YA WALIMU WA SAYANSI KUPEWA KIPAUMBELE SI TU KWENYE MIKOPO NA AJIRA BALI KATIKA MISHAHARA YAO, NYUMBA ZAO NA POSHO ZAO.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…