Kukubalika kwa CCM kuna sababu kuu tatu
- Chama kina sera nzuri
- Mgombea wake anakubalika na ana mvuto
- Kimuundo na historia ya kutetea wanyonge na kuleta maendeleo.
Sera za CCM ni zile ambazo zinaangalia matatizo ya jamii kama vile kutatua kero za barabara, shule , maji, umeme, ajira na ustawi wa jamii kwa ujumla. Hiyo huwezi kuikuta kwenye chama chochote.
Nikimwaangalia mgombea wa CCM kama vile padri, shehe, mchungaji, imamu , au mwanaharakati ambaye anaumizwa na matatizo ya wanajamii wanaomzunguka ametawaliwa na upendo, uvumulivu, subira, saburi, na shauku ya kuwasaidia wengine.
Kimuundo Chama cha Mapinduzi kina mtandao mkubwa kuliko mtandao wowote Tanzania si Vodacom, Tigo, Zain, Zantel, au TTCL yote hakuna mtandao kama CCM amabao unapatikana kuanzia ngazi ya chumba kwa chumba, shina kwa shina, mtaa kwa mtaa, Kata , wilaya, Mkoa , Taifa na sasa Kimataifa kina matawi Uingereza , Marekani . South Africa n.k. Hivyo Synovate na Redet utafiti wao uheshimiwe kwani CCM ina sababu nyingi ya kukubalika.