System (chuo) ya Sheng

pingli-nywee

JF-Expert Member
Joined
Sep 16, 2015
Posts
11,923
Reaction score
13,350
Vipi mraaya na mayout wa JF,

Kaa umekufia lugha hii yetu ya mtaa itabidi tuchapiane viserious juu yake. Mamwere wanengi wanabring pang'ang'a kuruka wakidai eti lingo ya sheng inafaa chochoro tu, eti ishaa beat! Wanengi wanadai iko down eti!Proof iko kuwa sheng haina limitations na inago places na pia ni identity ya wasee kibao Kenya na sanasana Nairobe. Mnadai jeiya mabudaboss? Temeni jo, bila mezesha any mamorio!
 
Hehe haina haja kuwapruvia any, ju wananyita ni lugha yetu, me nimekam kugundua sheng' huappreciatiwa Nai pekee, so better kubonga na wathii wanakuelewa kuliko kushinda mkibishana na rindi.
 
kweli but hii mraiya ya bongo wanajidai kuhate sheng but ni venye hawanyiti any wengine wao wameinoki but ni hard kwao,matoast
 
kuna msee mtz alinichapia vile iko ju,si eti wamelike swa yao sana ni venye wameconcentrate nayo design ya kunyita zingine ikawatoka.
 
Mwambie afike Nai tumpeleke kwanza the school of hard knocks, sheng' lugha ya mtaa, lazima azuru jiji kwanza
 
kweli mi nimechop na watz primo yote huko kajiado chuo yetu walikuwa mob than kenyans tulibishana sana ju ya ken-tz but haikuwa na hate i wonder ni jeiyaz all of a sudden wamekuwa na beef.
 
Pingli ebu nkumbushe jina ya hiyo primo.,ilikua kajiado hiii academy au?karibu na olkejuado high ata mi nlichop nao ki seco flani hapo ronga inaitwa nakeel sjui kama unairada...masangwenya ndo baoski hapa..
 
Na waliwanga na attitude gani na sheng'? Mliwanga mnabishana juu ya?
 
siunajua kubishana ki utoi,anthem yetu ni tamu shinda yenu,flag yetu iko sawa!nyinyi watz mbona hamjawai kuwa na tanzaniatta?ha!them days.
 
dem dayz nilikuwa bushboy bado hatukuwa tumehamia tao unasema nini nikiswitch swa ya bongo hutajua mi ni mkenya hata national anthem ya tz naichapa yote si nimekuchapia walikuwa mob than kenyans!
 
kuna mraiya hapo juu inabonga sheng ya Congo, maordinary place kaa arusha ma idhaa wanatry kuchapiana na sheng ndio ma toast wasishike rada. nakumbuka kuna time twitter kulikuwa na hashtag ya morio debate, kuna wadhi wanaboronja sheng ingine hauwezi ngam.
 
Hiyo amebonga huyo mkongomani sio sheng, hata sidhubutu kusema hivo manze...inaboo walahi!

Lakini haikosi hiyo sheng ya wadhii wa Arusha iko different sana na hii yetu. Sisi waky hatuwezi igich virahisi.
 
si siri sheng wameinoki wanachapiana hapa za ovyo but wanadai kuing'am but wapi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…