System ya Upigaji Kura Tanzania

System ya Upigaji Kura Tanzania

NullPointer

JF-Expert Member
Joined
Feb 7, 2011
Posts
3,461
Reaction score
2,273
Kwa muonekano wangu Tanzania ni nchi ambayo ina system ya ovyo sana ya kupiga kura, na hii ndio husababisha kila baada ya uchaguzi watu wanakua hawana kabisa imani na matokeo sio ya kuanzia ngazi za chini kabisa hadi kwenye urais, lakini hiyo siyo sababu pekee ya kwanini nasema matokeo hua sio ya ukweli 100% kua wananchi ndio wametaka hapana, wengi wanaopiga kura ni wamama, wababa na wazee, vijana wengi wamesambaa sehemu mbalimbali nchini, swala moja nalopingana nalo 100% ni ile mtu ukitaka kupiga kura inabidi urudi ulipojiandikisha kupiga kura, Nipo Arusha nafanya kazi, jina lipo Lindi, kazi ni ya kubangaiza, uwezo wa kwenda kupiga kura na kurudi utoke wapi? kama sio hivyo kuna process nyingi sana lazima usumbuke, kwa nini isiwepo system moja ya mtu kua na uwezo wa kupiga kura kutokea sehemu yoyote ile alipo nchini Tanzania?
Nikupe mfano wa Voting System ya nchi zilizoendelea kama Marekani, Brazil, China etc, na usiseme kua Tanzania haina hela au haiwezi kumudu maana hizi ni machine tu, na sio expensive kuzirun kama unavyofikiri, infact matumizi yanayotumika kwenye uchaguzi sasa hivi ndiyo hayohayo yanaweza kutumika kwenye system hii,
Angalia mfano wa picha hii

woman-screen-using-voting.jpg


Hizi machine zinakua nyingi katika Voting Stations ambazo zimesambaa nchi nzima, sasa watu wengi wanaweza wakawa na maswali na doubts nyingi, kwanza hii inatumia Card, ni electronic card kwa lugha rahisi kama kadi ambazo mtu hutumia kwenye ATM, kila mtu mwenye sifa ya kupiga kura anakua na kadi yake moja ambayo akiingiza kwenye machine na akafanikiwa kupiga kura mara moja (KUTOKA SEHEMU YOYOTE ILE NCHINI) basi kwa hiyo hiyo kadi akienda sehemu nyingine akitaka kupiga kura tena machine inagoma, tayari zina codes kwa wataalam wa computer wanajua ukishapiga kura machine inagenerate instruction kwenye card kua itakua inactive kwa muda flani hadi uchaguzi utakaofuata, na hiyo sio tu bado data inabaki kwenye mtandao mzima kua kadi yenye identity flani hairuhusiwi kupiga kura kwa hiyo hata ukisema unamachine ya kuweza kuclear hiyo instruction kutoka kwenye hiyo card bado ukiiweka itaonekana ishatumika sehemu nyingine. Hiyo ni security measure ya kwanza na kubwa sana, nyingine watu wanahofia kua vipi Hackers je hawawezi kuingilia hii system na kuchanganya hiyo mitambo, Hizi machine zinarun under private network, inshort ni kama vile haziko exposed na outside sytems ambazo zinaweza zikaleta vulnurebility kwa hackers, na bado zina backup systems zaidi ya moja, ambapo kila baada ya muda flani data ile ile inatumwa kwenye backup systems tofauti, mtu akichakachua moja zile nyingine hatojua zilipo, so still zile nyingine zitaweza kuprove data ambayo ni ya kweli maana baada ya sort nzima majibu yatakuja. Swala jingine ni je wale illeterate kabisa ambao hata kusoma na kuandika shida inakuaje, uzuri hizi mashine zinauwezo wa kuwa na picha pia, (no offense lakini, kama mtu hujui kusoma na kuandika hadi umri wa kupiga kura, hata sera za unayempigia kura si anaweza akakudanganya ukamchagua?)

Swala jingine, swala la watu kupigia kura kwenye shule madarasa yamebomoka ovyo, chini udongo udongo, hii nchi ina hela bna waache utani, kwa nini wasijenge voting stations nchi nzima, hiyo hela ipo kabisa, na kujenga voting stations kubwa kubwa watu wawe comfortable kwenda kupiga kura, ziwe very wide and open, machine nyingi kiasi kwamba watu waweze kuingia hata mia kwa wakati moja, AC inapuliza mdogo mdogo, na haya majengo sio kua yatagharimu bilioni kwa jengo moja, come on bna its just a hall ambalo tu limekua secured,
Naongelea kitu kama hiki
usa-campaign_-17.jpg


Tanzania ina hela ya kuweza kufanya haya kwa huu muda uliobaki hadi uchaguzi ujao, ni kitendo cha kutoa kadi kwa kila Mtanzania ambaye tayari ana sifa za kupiga kura, kadi ambazo ni Electronic ambazo zinaweza kusomeka katika hizi machine acha hizi tulizonazo sasa, na hiyo ni kujipanga tu na kufanya registration ya raia, kama sensa iliwezekana kwa muda mfupi, hii nayo yaweza kuchukua muda mrefu zaidi lakini still inawezekana sana tu, hii ndiyo njia itakayoondoa kelele za wananchi za kuibiwa kura kila mwaka, mbona kuna nchi baada ya uchaguzi hatusikii wanalalamika wizi wa kura?

Faida ya hii kitu ni kwamba kila kura moja inayoongezeka pia kuna system ya kutoa updates na kuzirusha hewani moja kwa moja, hakuna haja ya jamaa kwenda kutangaza kusoma kura kila mkoa ITV tena, zinakua zinarusha kwenye websites mbalimbali, ni kitendo cha mtu yeyote mwenye website anaweka extension tu, na zinakua katika form ya graphs ambazo zinapanda na kushuka kila update unavofanyika kutoka kwenye main server, Na mtu anaweza akafungua kitengo chochote wilaya yoyote na kuangalia nani anaongoza kwa kura hadi sasa, na nani yuko nyuma, nani kapita sehemu flani na nani kashindwa, kila kitu kinafanyiwa updates, hakuna kulaumiana..

Hayo ni maoni yangu Watanzania, naombeni mnipe Challenges nikubaliane na nyie kama hii system haitoweza kufanya kazi nchini, na kama ni challenge ambayo inaweza kua overcome ntajirahidi kuijibu kwa mujibu ninavyoweza kwa knowledge yangu ya teknolojia niliyonayo nikisaidiwa na great thinkers humu ndani.
 
Mkuu embu fikiria vizuri! Hivi ni kweli wafanye hivyo then wapoteze madaraka?
 
Mkuu embu fikiria vizuri! Hivi ni kweli wafanye hivyo then wapoteze madaraka?
Ni njia tu ya kuzuia kelele za watu kuiba kura kila uchaguzi, huwezi jua who will win, hii itakua a fair fight
 
Back
Top Bottom