T.O.T band kwenye mapokezi ya dreamliner,band yenu haikuwa ktk ubora wenu hasa kwenye upande wa vyombo...

T.O.T band kwenye mapokezi ya dreamliner,band yenu haikuwa ktk ubora wenu hasa kwenye upande wa vyombo...

FrankLutazamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2018
Posts
448
Reaction score
409
Mimi ni miongoni mwa mashabiki wenu,Mara ya kwanza nimewaona mwaka 1992,ktk ukumbi wa Urambo hotel-urambo kiingilio kikiwa tsh.500 watoto na tsh1000 wakubwa,Kopa ulikuwepo hata hayati kapt Komba aliimba na mlikuwa na kikundi cha sarakasi,nyoka aina ya chatu na taarabu

Pia nikawaona mwaka 1995 Tabora kwenye kampeni,Kopa ulikuwa ndani ya truck suite ya njano na wengineyo akina marehemu Banza.

Ktk mapokezi ya Dreamer sauti ilikuwa haisikiki vizuri,Vyombo havichuji mapigo ya mziki kabisa japo waimbaji mliimba vizuri

Uchangiaji wa maiki,nyie ndio jogoo wa Afrika Mashariki na kati hilo halina ubishi mpaka nje hukodiwa,Waswahili wanasema ukikaa na waridi lazima unukie,kwanini hamumuombi Anko Magu awanunulie maiki za kisaza zinazochuja sauti kwa ubora wa Kimataifa kama Mutukuzi au band za Afrika Kusini?kwanini mchangie maiki?

Nb:Anzisheni website au tovuti,muweke Picha tuone historia za wanamuziki wenu labda alikuwa band hii akahama akaingia hapa na Picha zenu,in ngumu kuwajua kwa sisi washabiki wenu.
 

Attachments

  • IMG-20180822-WA0016.jpg
    IMG-20180822-WA0016.jpg
    6.6 KB · Views: 23
Haya makitu/disco vigodoro ya ccm nayo ni jukwaa hili la intelijensia!?
 
Back
Top Bottom