Taa aina ya bulb inayowaka tangu mwaka 1901

Taa aina ya bulb inayowaka tangu mwaka 1901

Mjomba Fujo

JF-Expert Member
Joined
Oct 27, 2012
Posts
2,438
Reaction score
6,313
Taa aina ya bulb iliyopo katika state ya California imeendelea kuwaka tangu mwaka 1901 mpaka leo hii 2024, ilitengenezwa na Adolphe Chaillet muanzilishi wa kampuni ya Shelby Electric iliyoanzishwa mwaka 1890.

Kwa kifupi ni haijawahi kuzimwa, inashikilia rekodi za Guiness kama taa iliyosalia kuwaka kwa muda mrefu zaidi duniani.

Wanahakikisha inabaki on kwa maana ikizimwa inaweza isiwake tena.

View: https://www.youtube.com/watch?v=H6DbQeZbwAQ
 
Basi walitumia materials original kutengeneza hio taa , siku izi wanatengeneza feki kabisa
Hawatengenezi feki bali ni kitu yaitwa planned obsolescence, ni kama iphones na smartphones zingine zote, wanaweka muda maalum wa kuisha matumizi ili mnunue vipya tofauti na hapo watakosa mapato mengi hivyo basi kupelekea kukulazimisha mtumiaji wa mwisho kila baada ya muda fulani urudi dukani.
 
Mtengeneza taa hiyo hakutumia akili ya biashara.
Watu wote wa Dunia wangenunua bidhaa hiyo kiwanda cha huyo jamaa kingefirisika na kufungwa.
 
Taa aina ya bulb iliyopo katika state ya California imeendelea kuwaka tangu mwaka 1901 mpaka leo hii 2024, ilitengenezwa na Adolphe Chaillet muanzilishi wa kampuni ya Shelby Electric iliyoanzishwa mwaka 1890.

Kwa kifupi ni haijawahi kuzimwa, inashikilia rekodi za Guiness kama taa iliyosalia kuwaka kwa muda mrefu zaidi duniani.

Wanahakikisha inabaki on kwa maana ikizimwa inaweza isiwake tena.

View: https://www.youtube.com/watch?v=H6DbQeZbwAQ

Hata huku kiijini kwetu kuna koroboi haijazimika tangu 1960 upepo,mvu na jua bado inawaka!
 
Yaani huko umeme haujawahi kukatika kwa miaka yote hiyo? Vimbunga, vita havijawahi fika huko
 
Yaani huko umeme haujawahi kukatika kwa miaka yote hiyo? Vimbunga, vita havijawahi fika huko
Umeme unakatika kama kawaida ila imetengenezewa mazingira ya kutokukosa umeme.

Hata wewe ukiamua nyumba yako isikose umeme kwa kipindi cha miaka 20 mfululizo inawezekana ni mfuko wako tu.

Kuna Backup systems kama solar, battery, generators.
 
Daah mtu kagundua taa miaka 120 imepita harafu wewe mtumia bajaji na boda boda unasema hana akili aisee...mnapata wapi ujasiri wa kutukana wavumbuzi ?...
Huoni tofauti?
Mi nimeongea kibiashara wewe una hoja ya kisayansi.
Fikiria tena
 
Huoni tofauti?
Mi nimeongea kibiashara wewe una hoja ya kisayansi.
Fikiria tena
Mkuu mtu anagundua kitu ambacho leo hii Dunia inamzungumzia harafu wewe useme ajatumia akili kweli hapo umefikiri sahihi ? sidhani kama lengo la watu wenye akili ilikua kuuza wao wanagundua vitu wanavyoamini vinawezekana kama hivyo...
 
namna inawaka tu ni wazi hata hydrogen imekwisha humo ndani,umebaki waya tu kama mkaa.
 
Back
Top Bottom