Taa ya check engine inawaka na fundi amehangaika nayo bila mafaniko

duleikhufa

Member
Joined
Aug 26, 2022
Posts
6
Reaction score
10
Amani iwe nanyi.

Kuna hii taa ya check engine inawaka gari nimeipeleka kwa fundi wamehangaika nayo siku nzima ila bila mafaniko.

Na inawaka pale gari linapokuwa kwenye mwendo dk moja au mbili baada ya kuendesha.

Msaada kwa wandewa japo wa kifikra nijue naanzia wapi kutafuta ufumbuzi.

20230816_061834.jpg
 
Husemi ni gari gani halafu unataka msaada, watu wa vibaby walker mna shida sana.

Kwanza hiyo gari hujapeleka kwa mafundi, ulikuwa watu wamepaki magari mabovu wamevaa maovaloli unajuwa ni mafundi lakini hakuna mafundi hapo.

Hilo ni tatizo dogo, nenda garaji yenye diagnosis machine wacheki code ya hiyo sensor ubadili taa itazima.

Kwa kifupi shida ni sensor wanaita DTC P0500 kama sikosei.
 
Msaada kwa watu wenye ujuvi​

Sijui kama utapata msaada, kwani kichwa chako cha habari hakipo katika muundo wa kupata msaada kwa jinsi ulivyotumia neno ambalo halikustahili kuwepo katika kuomba msaada.

Ujuvi ni hali ya kujifanya kujua kila kitu, ni sawa na kusema ujuaji, ujeuri, ujuba, ufidhuli. Ungeandika, "Msaada kwa watu wenye ujuzi" nadhani ingekuwa sahihi.
 
P0500 ni speed sensor, na ni shida ya gearbox japo kwenye toyota huwa inawasha check engine kwa shida kama hizo pia sababu ya engine na gearbox kutumia module moja.

Lakini sababu ni nyingi kwa taa ya check engine bado huwezi kukisia.
 
Husemi ni gari gani halafu unataka msaada, watu wa vibaby walker mna shida sana.

Kwanza hiyo gari hujapeleka kwa mafundi, ulikuwa watu wamepaki magari mabovu wamevaa maovaloli unajuwa ni mafundi lakini hakuna mafundi hapo.

Hilo ni tatizo dogo, nenda garaji yenye diagnosis machine wacheki code ya hiyo sensor ubadili taa itazima.

Kwa kifupi shida ni sensor wanaita DTC P0500 kama sikosei.
Nashukuru sana kaka umenipa wazo.. ubarikiwe sana
 
Msaada kwa watu wenye ujuvi​

Sijui kama utapata msaada, kwani kichwa chako cha habari hakipo katika muundo wa kupata msaada kwa jinsi ulivyotumia neno ambalo halikustahili kuwepo katika kuomba msaada.
Ujuvi ni hali ya kujifanya kujua kila kitu, ni sawa na kusema ujuaji, ujeuri, ujuba, ufidhuli. Ungeandika, "Msaada kwa watu wenye ujuzi" nadhani ingekuwa sahihi.
Samahan mambo ya smartphone haya hasa ukiwa hujatulia na kutype.. naomba radhi kama limekukwaza
 
Hapana sijakwazika ila ndiyo hivyo tena tupo katika kusahihishana pindi tuonapokuwa tumekosea.
Nadhani wajuzi wameshakupa muongozo, tatizo lako litagundulika pindi gari ikifanyiwa scanning na vehicle diagnostic scanner.
 
Wamekuwa na msaada mkubwa sana. Nashukuru kwa hilo.
Mungu awabariki nyote
 
Back
Top Bottom