Sir robby
JF-Expert Member
- Jun 22, 2022
- 2,396
- 4,080
Wadau Katika pita pita zangu nimekuta na hii habari, binafsi siamini kama kweli Watendaji wa Serikali ya Katavi wamelikalia KIMYA suala hili hebu tusubiri tuone kama kuna Uwajibikaji kwa Wahusika au Mpaka Waziri Mkuu atoke Japan aende Katavi.
====================
Taa za disko zafungwa ICU Katavi
Wakati Mwenge wa uhuru ukimaliza kukagua na kutembelea miradi mbalimbali ndani ya Mkoa wa Katavi, umebaini dosari katika jengo la wagonjwa mahutututi katika hospitali ya wilaya ya Tanganyika, ambapo moja ya chumba kimebainika kufungwa taa za mwanga kama wa disko (dicso light).
Kiongozi wa mbio za Mwenge Kitaifa Sahili Geraruma, ameshangwazwa na wataalamu waliosimamia ujenzi wa majengo hayo kwa kutokuwa ya kisasa.
Akiendelea kubainisha dosari kiongozi huyo hajapendezwa pia na namna ambavyo mabomba yalivyotapakaa ukutani na kusema ujenzi huo sio wa kisasa.