Taa za sanamu maarufu "kristo mkombozi" zazimwa saa moja kumsupport vinicius junior

Taa za sanamu maarufu "kristo mkombozi" zazimwa saa moja kumsupport vinicius junior

carnage21

JF-Expert Member
Joined
Jan 24, 2023
Posts
591
Reaction score
1,382
Hapo jana taa za Sanamu Maarufu la “Kristu Mkombozi”(christ the redeemer) lililopo Rio de Janeiro huko Brazil zilizimwa kwa Muda wa Saa Moja hapo Jana ili kuonesha Mshikamano wa Watu wa Brazil na Mchezaji Vinicius Jr aliyefanyiwa Vitendo vya Ubaguzi huko Spain.

Pia wachezaji mbalimbali kama kylian mbappe,neymar n.k pamoja na makocha kama don carlo wa real madrid na xavi wa barcelona wameonyesha mshikamano wa pamoja kupinga vitendo vya kibaguzi nchini hispania.

FB_IMG_16848509539136215.jpg
 
Anapenda sana kucheza na jukwaa na haya ndo Madhara ya kucheza na jukwaa wakikurushia maneno kidogo tu lazima uhamaki
 
Tuache wivu huyu Dogo hana ubaya wowote sembuse angekuwa na mbwembwe uwanjani kama Ronaldihno si wengi mngepasuka vichwa acheni wivu dogo hana shida, Ila apate akili ahamie Manchester City au kwa mbali aende Man United
 
Wizara ya Michezo na Tamaduni za Dunia Mpo hapa.....

Hili nalo Mkalitazame
 
Tuache wivu huyu Dogo hana ubaya wowote sembuse angekuwa na mbwembwe uwanjani kama Ronaldihno si wengi mngepasuka vichwa acheni wivu dogo hana shida, Ila apate akili ahamie Manchester City au kwa mbali aende Man United
Si bora aende flamengo ya kwao brazil kuliko kwenda man u
 
Back
Top Bottom