TAALUMA MKOA WA KAGERA INAPOROMOKA KWA KASI YA AJABU

TAALUMA MKOA WA KAGERA INAPOROMOKA KWA KASI YA AJABU

Seth seth

Senior Member
Joined
Jan 2, 2022
Posts
106
Reaction score
150
Mkoa wa Kagera ni miongoni mwa mikoa michache hapa nchini iliyojijengea heshima kubwa katika utoaji wa elimu Bora na wataalamu wengi katika fani mbalimbali. Ndiyo maana hata Sasa hivi ukimuuliza mtanzania yeyote akutajie mikoa inayoongoza kuwa na wasomi wengi lazima Kagera ni mkoa mmojawapo.
Jambo la ajabu ni kwamba kwa miaka ya hivi karibuni mkoa huu yameporomoka kitaaluma Hadi kushika nafasi za mwishoni. Sababu zinazotajwa kuchangia Hali hiyo ni nyingi lakini baadhi nihizi zifuatazo;
1. Uvamizi wa wanasiasa katika taaluma. Siku hizi wanasiasa ndio wanaowapangia wataalamu Nini Cha kufanya hata Kama mwanasiasa huyo kaishia darasa la Saba. Kwa mfano siyo ajabu kukuta kiongozi wa kisiasa Kama vile diwani, mkuu wa wilaya, mkuu wa mkoa akimshururisha mtaalamu wa elimu Nini ha kufanya hata Kama ni kinyume na taratibu. Endapo kiongozi wa elimu atakaidi basi atatengenezewa mizengwe ya hapa na pale hatimaye atasimanishwa kazi,atashushwa cheo au kufukuzwa kazi kabisa hivo viongozi wa elimu wanaamua kuteleleza take wanatotaka wanasiasa hata Kama ni upuuzi ili kulinda kibarua chao mwisho wa siku kiwango cha elimu kinaporomoka.
2. Imegundukika kwamba walimu wakuu wengi hutumia muda mwingi kusimamia miradi ya ujenzi wa miundombinu ya shule hivyo kuishindwa kusimamia taaluma.kwa utaratibu kazi hiyo ilitakiwa ifanywe na ofisi ya mhandisi wa wilaya lakini unakuta mwalimu ndiye mhandisi ndiye mhasibu ndiye mgavi kila kitu ni yeye. Na endapo kazi ya ujenzi unashindwa kukamikika au ikajengwa chini ya viwango walimu hutishiwa maisha , hufungwa jera na kuazimika kulipa fidia ya kilichoungua ilihali wao siyo wataalamu wa ujenzi. Mwisho wa siku wanafunzi wanavaki bila kusimamia kitaaluma ipasavyo matokeo take no kuporomoka kwa kiwango cha elimu
3.Baada ya matokeo ya mwaka Jana kuwa mabaya zaidi nikama mkoa mzima umechanganyikiwa. Taarifa zinaeleza kwamba Sasa hivi walimu wanalazimishwa kufanyisha mitihani wanafunzi kila wiki kila mwezi na kuwasilisha matokeo mkoani. Pia walimu wanalazimishwa kufundisha Hadi siku za jumamosi na Jumapili kinyume kabisa na kanuni za utumishi. Wanafunzi hawafundishwi ipasavyo kwa sababu muda mwingi wanakuwa wakifanyishwa mitihani inayoambatana na vitisho vingi kutoka kwa viongozi wa elimu . Mbaya zaidi mitihani yenyewe walimu hulazimika kuiandika ubaoni kwa chaki kwa kukosa gharama za kuichapisha kwa kuwa ni mingi na lazima yote ifanyike. Kama Hali utaendelea kuwa hivo pengine tunaweza kushuhudia mkoa huu unoongoza kuwa na maprofesa wengi duniani ukiendelea kuburuza mkia.
TAALUMA ya ualimu ni Kama taaluma zingine lazima iheshimiwe.unawezakumlazmisha mwalimu afanye vile wewe unataka kwa mabavu kwa kuwa umeshikilia mpinilakini ukapuuza kumpa nafasi ya kumsikiliza matokeo yake utayaona muda siyo mrefu. Wapi uliona shule zinafungua mwaka wa masomo kwa kufanya mitihani wakati wanafunzi hawajafundishwa? Majibu watayatoa wapi? Mada zitaisha lini?
4. Kuna hili swala la mtaala mpya. Hivi viongozi wa Elimu wanajua kwamba Hadi Leo hii MWEZI wa tatu shule hazina vitabu vya mtaala mpya? Wanajua kwamba watoto wa darasa la tatu, la nne, kidato Cha kwanza hawasomi baadhi ya masomo kwa kuwa hakuna vitabu? Kidato Cha kwanza wanalazimishwa wachague michepuo ya masomo ya Sanaa au ya sayansi ambayo hata hawayajui Wala hawajawahi kusoma??eti wakawaulize wazazi wao wawashauri ni masomo yapi wayasome huku baadhi ya wazazi hawajui kusoma Wala kuandika???ety mtoto wa form one aulizwe Kama anapenda kusoma SoMo la kemia au fizikia wakati mtoto mwenyewe hajawahi hata kulisikia SoMo Hilo???
Viongozi wengine wanawaambie walimu eti wadaunilodi vitabu vya mtaala mpya kutoka kwenye mtandao ndio wafundishe kweli??
Mlikuwa na dharula gani kuharakisha huu mtaala mpya kama mlikuwa bado hamjajipanga?
 
Kwamba Kagera hawana akili naturally?
 
Back
Top Bottom