taaluma ni nzuri, na haitofautini na taaluma nyingine za social science kwa mawazo yangu.
Kinachoboa katika utendaji wa kipolisi, ni pale tu jeshi linapokuwa na uhusiano na siasa. IJP huteuliwa na mwanasiasa. Unapoteuliwa na mwanasiasa, lazima kuna expectation kadhaa anazozitarajia kutoka kwako. Ni katika kutimiza expectation ya bosi aliyekuteua basi unaingilia haki za watu wengine hivyo unaharibu.
Kwa upande mwingine, makamishina wote file zao ziko kwa mkuu wa kaya. Mkuu wa kaya anaamua nani awe kamanda nani awe mkuu wa kitengo fulani. Katika kutekeleza hilo, makamishina wamejikuta wakitekeleza hadi amri za bosi, kwa wanandamu tuliowengi, tunaamini kuwa tupo ili tule vizuri, na kwa kuwa mkuu wa kaya anakuwezesha kula vizuri, utalinda sana lindo lako hatimaye UNAWAKAMHANDA WATU wengine wanaodai uwajibikaji wa serikali ya bosi wako.
Viongozi waandamizi kuanzia ASP hadi SSP, nao kwa upande mwingine wanaendekeza yaleyale kwa kuamini kuwa wanapokuwa wamemsaidia mkuu wa kaya na chama chake katika nafasi nzuri, basi kuupata u commisioner inakuwa ni rahisi na kupata madara mengine ya kipolis.
Kujibu swali lako, Taaluma ya POLICE SCIENCE na taaluma nyingine ndani ya jeshi kama sheria, sociology, ualimu na nyingine nyingi zitakuwa na maana iwapo tu:-
(a) Tutaweza kutenganisha siasa na utendaji wa umma. Hii ni kusema kuwa kama ni viongozi wa polisi watokane na sifa zilizoainishwa au waachiwe polisi wenyewe kuwapigia kura.
(b) Viongozi wa wizara nao wataajiriwa kwa sifa zao ni wala si kwa nasaba walizonazo na watawala. hapa namzungumzia mkurugenzi na waziri wake.
Yote haya yatafanikiwa iwapo wananchi watayadai katika katiba mpya na yakasimamiwa.