SoC01 Taaluma ziheshimiwa maendeleo yapatikane

SoC01 Taaluma ziheshimiwa maendeleo yapatikane

Stories of Change - 2021 Competition

GoJeVa

Member
Joined
Sep 15, 2021
Posts
41
Reaction score
60
TAALUMA ZIHESHIMIWE MAENDELEO YAPATIKANE.
Kwanza kabisa tujiulize maswali mawili, Taaluma ni nini na maendeleo ni nini?.

Taaluma ni ujuzi ambao mtu ameupata kutokana na mafunzo maalumu ya elimu kwa ajili ya kutoa huduma kwa jamii. Mfano wa taaluma ni kazi ambazo watu huitaji kusomea au kujifunza kwa kupitia mafunzo maalumu, kama vile;
*Ualimu (hapa mtu hupitia mafunzo ya ualimu).
*Uwakili (hapa mtu hupitia mafunzo ya sheria ikiwemo na mafunzo ya uwakili).
*Uhasibu (hapa mtu hupitia mafunzo ya uhasibu).
*Udaktari (hapa mtu hupitia mafunzo ya udaktari).
Zilizohorodheshwa hapo juu, ni mifano michache tuu ya taaluma. Baada ya kuona maana ya taaluma sasa tuangalie maana ya maendeleo;

Maendeleo ni mabadiliko chanya yanayolenga kuboresha hali za maisha katika nyanja mbali mbali kama vile; kiuchumi, kijamii na kisiasa.

Katika nchi nyingi zilizoendelea wanathamini sana mchango wa taaluma katika kuleta maendeleo, mfano nchi kama China na Japan wamejitahidi kuwekeza katika teknolojia kwa kuwa na wataalamu wengi na wabobezi katika suala hilo la teknolijia, na ndio maana kwa sasa nchi kama China imeendelea sana kiteknolojia.

Hivyo tunaona wanazalisha vitu kama simu za mikoni na kusambaza karibia dunia kote, pia wanazalisha vitu kama televisheni, pasi za umeme, majokofu. Pia, tunaona nchi kama India imewekeza kwa kiasi kikubwa katika mambo ya tiba hasa tiba za binadamu ndio maana si ajabu tukisikia mtu anaenda kutibiwa India. Hii ni kwa sababu nchi hiyo ina madaktari bingwa, kutokana na kuwekeza kwenye taaluma hiyo.

Sasa tuangalia mchango wa wa taaluma katika nchi yetu ya Tanzania katika kuleta maendeleo;
Nchi ya Tanzania kwa upande fulani tunawez sema haithamini sana taaluma za watu, sijui ni kasumba au laa. Kuna mfano mmoja halisi ambao niliwahi shuhudia ndani ya nchi yangu ya Tanzania. Ilikuwa mwaka 2018 nilikuwa nafundisha shule mojawapo ya sekondari ya mtu binafsi, katika shule hiyo nusu ya walimu walikuwa hawajasomea taaluma hiyo. Bali walifanya kazi hiyo kwa mazoea, kwa sababu wengine walikuwa ni wahitimu wa kidato cha sita na wengine walikuwa wamesomea fani zingine kama vile uhasibu na uandishi wa habari. Huo ni mfano mmoja tuu, lakini ukifatilia kwa karibu shule nyingi za watu na taasisi binafsi walimu wao wengi hawajasomea taaluma hiyo ya ualimu bali wapo huko ili kuendesha maisha, bila kujali madhara atakayo pata mwanafunzi na taifa kwa jumla.

Katika hili wakaguzi wa elimu na wathibiti ubora ndani ya nchi yetu inabidi wajitathimi. Nakumbuka kuna siku nikiwa katika hiyo shule nikiwa kama mwalimu, walikuja wakaguzi wa elimu. Wakaguzi hao walikagua vitu vingine ikiwemo taaluma lakini chakushangaza ilifika muda wa kugagua vyeti vya walimu waliitwa pembeni na mwenye shule na hapo ukaguzi wa vyeti ukawa umezimwa.

Je? Tunatengeneza taifa la aina gani?, wanafunzi watakaohitimu watakuwa mahiri?, au wataishia kukanyaga haki za watu na kuua watu?.

Hapo nimeongelea upande wa elimu, ambao nimeshuhudia kwa macho yangu. Je vipi? kuhusu wahandisi wetu, waandishi wetu wa habari, wauguzi wetu ni kweli wengi wao sio makanjanja?.

Ni vizuri kwa serikali yetu, itambue kuwa taaluma ni muhimu sana kwa maendeleo ya nchi. Hivyo lazima ihakikishe wanaofundisha shuleni (shule binafsi na za serikali) ni waalimu wenye taaluma hiyo, pia waandishi wa habari wanaofanya kazi hiyo ni vizuri wahakikishe wana taaluma hiyo.

Vivyo hivyo wanasheria, wahandisi, wauguzi na wengineo lazima wafanye kazi walizoziomea kikamilifu. Hii itatusaidia kujenga taifa lenye maendeleo endelevu.
AHSANTE.
 
Upvote 7
Courses/taaluma zinazotolewa ziwe zinalenga katika kuchochea kutumia resource tulizonazo katika jamii yetu ili matumizi ya taaluma yawe ni kubadilisha mazingira yetu kwa kuyaboresha na kuibua vitu vipya ili kurahisisha maisha, kuongeza ajira, kipato na kuinua uchumi wa taifa kwa ujumla
 
Courses/taaluma zinazotolewa ziwe zinalenga katika kuchochea kutumia resource tulizonazo katika jamii yetu ili matumizi ya taaluma yawe ni kubadilisha mazingira yetu kwa kuyaboresha na kuibua vitu vipya ili kurahisisha maisha, kuongeza ajira, kipato na kuinua uchumi wa taifa kwa ujumla
ahsnte kwa mrejesho mzuri.
 
Hujaongelea suala la nafasi za kisiasa, Daktari wa binadamu tena wakati mwingine ni bingwa anaenda kuwa mbunge au anateuliwa kwenye nafasi ya kisiasa ambako udaktari wake hataweza kuutumia!
 
Hujaongelea suala la nafasi za kisiasa, Daktari wa binadamu tena wakati mwingine ni bingwa anaenda kuwa mbunge au anateuliwa kwenye nafasi ya kisiasa ambako udaktari wake hataweza kuutumia!
Ahsnte kwa mrejesho na nyongeza nzuri.......nitaandaa makala nyingine kwa upana zaidi, kutokana na nyongeza mbali mbali nilizopata hapa.
 
Back
Top Bottom