Mwanakili90
JF-Expert Member
- Nov 24, 2010
- 1,568
- 245
mi naichukia na siipendi.Hivi humu JF kuna wapenzi wa Taarab kweli? Mimi napenda sana Taarab aisee. Napenda midundo yake. Napenda jinsi nyimbo zake zilivyo ndefu. Unasikiliza hadi unaridhika.
Napenda jinsi watunzi na waimbaji wake wanavyotumia ujuzi wa lugha kufikisha ujumbe. Hususan napenda jinsi sitiari zinavyotumiwa.
Aah mirindimo ya Taarab swaaafi sana.
Na ndiyo siyo inakuwajeWewe ni demu?
mi naichukia na siipendi.
Unapenda taarabu, then hujui Mayasa ni jinsia gani? Shame on you!
Mimi pia naipenda taarabu sana huchoki kucheza kabisa halafu maneno yana ujumbe
Swaafi sana
kama unaweza mpe asitoroke nyumbani, kama unaweza mume asibanduke chumbani,
Muandalie mapishi akishiba ajirambe, awakomeshe wazushi apitapo ajigambe
Huwa unakwenda wapi.......Travertine au???
Sikosagi mimi hapo. Halafu Jahazi wanazindua vitu vipya Jumapili ya Pasaka....I can't wait aisee. That Mzee Yusuf ni mwisho hahahahaaaaaaa big up Jahazi Modern Taarab
Ka ni njemba halafu anajiita Mayasa, basi ana walakini huyo...Wewe kila jina la mwanachama wa JF unaijua jinsia yake ya kweli? We ngumbaru kweli wewe...yaani hujui kuwa JF ni chaka la kuficha utambulisho wa watu? Hebu nipishe huko ebo!!!!
NN mimi napenda sana taarab ingawa si nyimbo nyingi saana.mashairi yake yamepangwa vzr na huliwaza na kuburudisha muda mwingi na huku nyingi zikituongezea ujasiri wanawake dhidi ya wakaka na wanaume wengne.angalia hiki kipande 'kupendwa bahati yangu si mzizi kutumia,asili na jadi yangu wangu kumringia. Na 'penzi hili siri yangu kazi bure unanuna,yeye ametua kwangu mimi haswa namkuna.amependa umbo langu nini kinachokutona,amependa umbo langu nn kinachokutona. kwa ujumla taarab iko muzuri sana
chakula nnapikiwa, nnawekewa mezani,
nikila nnapepewa, kishuke vema tumboni,
sigombwi mimi, nnadekezwa,
na nikiumia napulizwa,
kufanya utundu nnakatazwa,
siwahi kusema, nnaulizwa,
nikiwashwa hunikuna na muwasho ukaisha,
na maradhi nnapona, presha ananishusha,
shuu shuu shusha, ananishusha