- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Naona kama CHADEMA wameenza kutusaliti Gen Z
Yaani watu tunajua tupo pamoja Oktoba 29, 2025 kupambania G Wagon na Royce alafu wanaleta tena siasa za CCM
Wakuu ebu iangalieni hii kabla sijachanganya mambo
Yaani watu tunajua tupo pamoja Oktoba 29, 2025 kupambania G Wagon na Royce alafu wanaleta tena siasa za CCM
Wakuu ebu iangalieni hii kabla sijachanganya mambo
- Tunachokijua
- Ipo taarifa inayosambazwa mtandaoni ikidawa kutolewa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) ikidaiwa kuwa ni wito amani kwa watanzania, vilevile zimetumika grafiki zenye utambulisho wa vyombo mbalimbali vya habari ambavyo vinadaiwa kuripoti taarifa hiyo.
Je, ni kweli taarifa hiyo imetolewa na CHADEMA?
Ufuatiliaji wa kimtandao uliofanywa na JamiiCheck kwa kutumia utafutaji wa maneno muhimu (Key words search) umebaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli, bali imetengenezwa na wapotoshaji kwani haijachapishwa katika kurasa rasmi za CHADEMA.
Aidha grafiki zilizotumika kusambaza taarifa hiyo ni za kughushi kwani hazijachapishwa na vyanzo hivyo (Millard Ayo, Jambo TV, Nipashe Digital) kama inavyoonekana. Grafiki hizo zina mapungufu kadhaa ikiwemo miundo tofauti na inayotumiwa na vyanzo hivyo.
Kadhalika Taarifa iliyodaiwa kutolewa na CHADEMA ina mapungufu kadhaa ikiwemo matumizi ya lugha mbili kwenye taarifa moja, kukosewa kwa siku, badala ya Jumatatu imewekwa Jumanne Septemba 22, 2025. Mapungufu haya yote yanadhihirisha kuwa taarifa ni ya kutengenezwa.