Waandishi Wetu
MCHUNGAJI Ambilikile Masapila anayetoa tiba ya magonjwa sugu katika Kijiji cha Samunge, Loliondo amewataka wagonjwa kuendelea kutumia dawa za hospitali hata baada ya kunywa dawa yake.Akizungumza kijijini hapo jana, Mchungaji Masapila alisema hakuna madhara kwa mgonjwa kuendelea na dawa zake za awali hata baada ya kunywa dawa yake na kwamba si vyema kuacha ghafla kutumia dawa hizo.Hii dawa yangu inatibu, lakini haizuii kunywa nyingine, unaweza kunywa na ukiona umepona kabisa usiendelee kunywa dawa hizo, alisema.
MWANANCHI.
Habari hii imeandikwa na Salim Mohamed, Neville Meena na Mussa Juma, Samunge.