SoC03 Taarifa kuwa Watanzania wanaotumia nishati ya umeme nchini ni million 4.4 kati ya million 60 sio kweli

SoC03 Taarifa kuwa Watanzania wanaotumia nishati ya umeme nchini ni million 4.4 kati ya million 60 sio kweli

Stories of Change - 2023 Competition
Joined
Aug 11, 2022
Posts
7
Reaction score
2
Akizungumza Mkurugenzi wa Shirika la Umeme Tanzania [ TANESCO ] Ndg. Maharage Chande, amesema kukamilishwa kwa Bwawa la Nyerere [ JNHPP ] hakutapunguza gharama ya umeme nchini kwa sababu Shirika litashindwa kujiendesha.

Amesema, mpaka sasa wateja wahudumiwao na [ TANESCO ] ni Milioni 4.4 wakiwemo Wateja wa Majumbani na wa Viwandani. Pia, gharama za uzalishaji zimepanda kutoka Tsh. Trilioni 1.5 Mwaka 2020/21 mpaka Tsh. Trilioni 1.6 Mwaka 2021/22.

Matumaini ya Watanzania tena yametoweka. Wakati mchakato wa ujenzi wa bwawa hili, Lengo lilikuwa kupunguza gharama za umeme Nchini kwa Watanzania ila naona hili bwawa linanaweza kuwa chanzo cha upandishaji wa umeme tena Nchini. Kinyume na matarajio ya Watanzania. Serikali ya awamu ya Tano ilituaminisha hilo leo awamu ya sita aimelikataa hilo.

Sitaki kuamini kabisa kabisa kuwa watu milioni 4.4 ndio WANATUMIA umeme Nchini. Sasa Serikali inaposema Umeme umefikia Asilimia 76% Ya Watanzania wote Nchini ndio hao 4.4 milioni kweli.

Sina hakika kabisa kama TANZANIA kwa sasa inahitaji wasomi na hawa wanaojiita wataalam kuongoza hii nchi.

HAIWEZEKANI MTU ATUUZIE AINA HII YA UONGO RAHISI SANA. HII NI AIBU SANA.

YAANI WATANZANIA MILIONI 55 HAJUI UMEME? HUYU MTU AOMBE RADHI SERIKALI NA KWA WATANZANIA KIUJUMLA MAANA KATUDANGANYA. HUYU MTU AWAJIBISHWE KISHERIA KWA KUDANGANYA UMMA WA WATANZANIA.

Halafu wakipanda majukwaani wanasema 80%ya nchi umeme umefika. Sasa hivyo vijiji uliko umeme umefungwa kwenye miti?. Hawa binafsi nahisi wanajua Nchi ina watu 6 milioni ndio maana 80% ni 4 milion.

Hakuna haja ya kushangaa. Maana gharama zake zinaweza kuwa zimeongezeka maradufu kuliko makadilio yake ya awali. Nijuavyo, mpaka Medard Kalemani anatoka kwenye wizara mradi ulikuwa asilimia 81. Kwamba ulibakiza miezi tu uanze kufanya kazi. Baada tu ya kutoka tukaanza kuambiwa kuwa mradi ulikuwa asilimia 37. So to cover the cost lazima tuanze kupewa report za uongo.

Maana yake ni kwamba, gharama hewa ziliingizwa katika mradi. Na gharama hizo haziwezi kurudi bila kupandisha bei ya umeme ili kupata hela ya kulipa madeni.

Mradi huu unanikumbusha mradi wa reli (sgr) ya watu wa Kenya. Matarajio na matumaini juu ya mradi wao yalikuwa makubwa mithili ya miujiza. Lakini miujiza walokuja kuishuhudia ni miujiza ya kukatisha tamaa.

Ni kwamba, badala ya reli kushusha gharama za maisha, ikapandisha mara dufu. Matokeo yake wamebaki kuwa watu wa kushinda barabarani na vituo vya polisi wakilalamikia kupanda bei ya unga na maisha kwa ujumla.

Duniani kuna mambo. Na ukitaka kuyajua mambo yenyewe, tembelea nchi za Afrika ukidurusu mifumo yake ya uongozi. Na kimsingi mambo yenyewe ndiyo haya.

Serikali inapotoa ahadi hasa kwenye hii miradi mikubwa basi ziwe za kweli. Maana watanzania walio wengi wanaamini kuwa mradi watanesco wa kule rufiji ukikamilika bei ya umeme itashuka. Sasa kwa alivyosimama kiongozi na kuongea vile imaana umeme hauta shuka bali utaongezeka.

Serikali inabidi itambue kuwa umeme ni chachu ya maendeleo ya vijiji na miji inayokua nchini. Kunapokua na umeme eneo fulani basi inavutia wawekezaji na itachochea maendeleo ya eneo husika.

Kwa bei ya umeme iliyopo sasa hivi ni kubwa kwa mtanzania uniti moja ni Tsh 350 sasa kwa bei kama hii inamuumiza mfanyabiashara mdogo. Hali hii itampelekea mtanzania wa hali ya chini kushindwa kuendesha biashara kutokana na gharama kubwa ya umeme.

Serikali inabidi itafute vyanzo vingine mbadala vya kuzalishia umeme. Ili kufanya nchi iwe na umeme wa kutosha. Nchi zilizoendelea zinatumia umeme wa upepo kwasisi inawezekana. Mikoa iliyomo katika mwa tanzania inamuinuko na upepo wa kutosha tunaweza kufungu mitambo na umeme ukaongezeka nchini.

Serikali iwajibike kuzuia au kuondoka kukatika katika kwa umeme. Kukatika kwa umeme kusababisha hasara kwa wafanyabiashara na wamiliki wa viwanda au offisi. mfano umeme unapokatika na ukiwa na generator la 450 kvA ndani ya lisaa 1 linaweza kutumia mafuta lita 75 na kuendelea. Kumbuka lita ya mafuta diesel 2740 na kuendelea kwa lisaa limoja generator likitumika litagharimu Tsh 205500. Ukizingatia hii pesa kama angenunua uniti za umeme basi angepata uniti nyingi sana.

serikali inabidi iwawajibishe wafanyakazi walio katika sekta ya nishati na wameshindwa kutatua matatizo yaliyomo kwenye sekta ya nishati.

Serikali iwajibike kujizatiti katika nishati na kuondoa watu wasiokua na ufanisi katika sekta ya nishat. Itasaidia kupunguzia mzigo kwa wananchi na itavutia wafanyabiashara wakubwa na wawekezaji. Kuweza kuja tanzania kuwekeza kutokana kuwa na uhakika kwamba kunaumeme wa kutosha.

Mwandishi Mr Og
 
Upvote 0
Back
Top Bottom