Nipende kuchukua nafasi hii kuwashukuru kwa ujenzi unaoendelea ya barabara ya lami hapa Mtaa wa Mwananchi Kata ya Mahina. Mkandarasi JASCO anatakiwa kujenga madaraja madogo yanayoingia kwenye makazi ya wenye nyumba kando kando ya barabara hiyo. Baadhi ya madaraja hayo amekwishayakamilisha na baadhi bado hajayakamilisha na inawawia vigumu sana wenye makazi kupita na kuingia kwenye makazi yao na pia kuingiza magari yao. Sasa yapata miezi mitatu tunapata adha hii na vyombo vyetu vya usafiri tunayaacha nje kwa kukosekana njia ya kuingiza hivyo vyombo. Mfano hai ni nyumba Na.6 mpaka sasa hawajakamilisha daraja la kuingia kwenye makazi ya mwenye nyumba. Tunawaomba kazi hii ikamilike ili tupate urahisi wa kuingia kwa urahisi kwenye makazi yetu na kuingiza vyombo vyetu vya usafiri kwenye makazi yetu.