Taarifa kwa Umma Kuhusu Ndege ya Precision Air (PW 602) Iliyositishwa Kutua Dodoma Ikitokea Dar es Salaam Mei 1, 2023

Taarifa kwa Umma Kuhusu Ndege ya Precision Air (PW 602) Iliyositishwa Kutua Dodoma Ikitokea Dar es Salaam Mei 1, 2023

KING MIDAS

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2010
Posts
8,589
Reaction score
16,936
TAARIFA KWA UMMA KUHUSU NDEGE YA PRECISION AIR (PW 602) ILIYOSITISHWA KUTUA DODOMA IKITOKEA DAR ES SALAAM TAREHE 01/MAY/2023

Tarehe 1 Mei 2023, Ndege ya Precision Air No. PW 602 iliondoka uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 18:11 (saa za ndani) kwa safari ya saa moja kuelekea Dodoma, ikiwa imebeba abiria 72.

Ndege hiyo ilitarajiwa kutua katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma takriban saa 19:13 ambao ni zaidi ya saa za kazi katika Uwanja wa Ndege wa Dodoma, yaani 18:30 (saa za ndani).

Kwa sababu ya kizuizi cha miundombinu kulingana na nambari za taarifa kwa watumiaji wa anga "Notice-To-Airmen" (NOTAM) B0027/23, BO026/23, BO025/23, BO024/23 na B0023/23, kuwa Uwanja wa Ndege wa Dodoma hufanya kazi baada ya Jua kuchomoza na kabla ya Jua kuzama na kulingana na Uchapishaji wa Taarifa za Anga GEN 2.7-4 ya tarehe 5 Januari 2017.

Muda wa saa 18:48 (saa za ndani) Rubani aligeuza ndege kurudi JNIA baada ya kupokea muongozo kutoka kwa muongozaji ndege angani.

Uchunguzi wa awali ulibaini kuwa kulikuwa na dosari za kiutendaji, na Mamlaka inaendesha uchunguzi zaidi ili kubaini uwezekano wa kutofuata Sheria ya Madai Kanuni za Usafiri wa Anga.
Mamlaka itachukua hatua zinazofaa kulingana na sheria zinazotumika.

Mamlaka inapenda kuwahakikishia wananchi kuwa safari ya ndege iliyogeuzwa njia ilifanyika kwa kuzingatia, taratibu za uendeshaji zinazotumika na hakuna wakati ambao usalama wa ndege na waliokuwemo ndani ya ndege waliathirika.

Imetolewa na:
Hamza Johari,
Mkurugenzi Mkuu,
Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)
 
Miaka 60 ya Uhuru
uwanja wa ndege dodoma yalipo makao makuu ya nchi yetu

serikali ya CCM inayokusanya Kodi na tozo kila kukicha imeshindwa kabisa kufunga taa uwanjani ili ndege ziweze kutua usiku[emoji848][emoji26]
 
Daaaa!!hii nchi huwa vituko haviishi!!!ina maana toka inaruka kutoka dar,rubani alikuwa halijui hilo na waongoza ndege?hapo kuna kitu kimejificha,huenda siku zote muda huo huwa ndege zinaruhusiwa ila kwa siku hiyo kulikuwa na kizingiti kingine kipya kilichojitokeza.Yaani wachome mafuta bure!!!??
 
Back
Top Bottom