Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,278
- 797
Taarifa kwa Umma kuhusu uapisho wa Mbunge Mteule Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb).
Spika wa Bunge Mhe. Dkt. Tulia Ackson (Mb), atamuapisha Mbunge Mteule Mheshimiwa Balozi Mahmoud Thabit Kombo (Mb), kesho tarehe 25 Julai, 2024. Tukio hilo litafanyika saa 9:00 alasiri katika Ofisi Ndogo ya Bunge iliyopo Jijini Dar es Salaam.
Mheshimiwa Kombo aliteuliwa kuwa Mbunge tarehe 21 Julai, 2024 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Samia Suluhu Hassan
Uapisho huo utafanyika kwa mujibu ya Kanuni ya 30 (2)(b) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Februari, 2023. Kanuni hiyo inaeleza kwamba Mbunge kabla ya kuanza kazi ataapishwa katika eneo litakalopangwa na Spika iwapo hakuna Mkutano wa Bunge unaoendelea na baadaye Spika atatoa taarifa Bungeni kwenye Kikao cha Kwanza cha Mkutano wa Bunge unaofuata.
Imetolewa na:
Kitengo cha Mawasiliano na Uhusiano wa Kimataifa,
Ofisi ya Bunge, 10 Barabara ya Morogoro,
S. L. P 941, 40490 Tambukareli,
DODOMA.
24 Julai, 2024.