Taarifa kwa Umma toka Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi

CompaQ

JF-Expert Member
Joined
Dec 31, 2012
Posts
281
Reaction score
134
JAMHURI YA MUUNGANO WATANZANIA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI UFAFANUZI KUHUSU KUPITIWA UPYA KWA MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE MWAKA 2012

Mnamo tarehe 03 Mei, 2013 Serikali kupitia Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa WiliamLukuvi (Mb) ilitoa Kauli ya Serikali Bungeni Kuhusu Taarifa ya Awali ya Tume ya Taifa ya Kuchunguza Sababu za kushuka kwa ufaulu wa Mtihani wa Kidato cha Nne Mwaka 2012.

Kauli ya Serikali ilielekeza kuwa matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha Nne mwaka 2012 yafutwe na yaandaliwe upya kwa kutumia utaratibu uliotumika mwaka 2011 ili Wanafunzi hao wawe katika mazingira
yanayofanana na ya wenzao wa miaka iliyopita kwa kuwa mfumo uliotumika mwaka 2012 katika kupanga matokeo na madaraja ni tofauti na ule uliotumika mwaka 2011 na miaka iliyotangulia.

Kwa kuzingatia mapendekezo ya Tume na Maelekezo ya Baraza la Mawaziri, Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, kwa mamlaka aliyonayo chini ya Sheria ya Baraza la Mitihani Tanzania, kifungu cha 20, sura 107 ameliagiza Baraza la Mitihani la Taifa kupitia upya Matokeo ya Mtihani wa Kidato cha Nne mwaka 2012. Aidha, imeagizwa kwamba matokeo hayo yaandaliwe kwa kutumia utaratibu uliotumika mwaka 2011.

Serikali haikuagiza kufanyika upya kwa mitihani hiyo na wala haikuagiza kusahihishwa upya. Hivyo, Serikali inapenda kuwahakikishia wananchi kwamba hapatakuwa na zoezi la kurudia usahihishaji wa mtihani huo kwa sababu hakuna dosari zilizobainishwa kwenye usahihishaji wa mitihani hiyo.

Alama za watahiniwa ambazo zimehakikiwa zipo tayari, kitakachofanyika ni kwa Baraza la Mitihani kutumia alama hizo kuchakata matokeo upya kwa kutumia viwango vya ufaulu vilivyotumika mwaka 2011.

Utaratibu ambao umekuwa ukitumika tangu mwaka 1973 wakati Baraza lilipoanzishwa, ni wa kuweka viwango vya ufaulu kila mwaka kwa kuzingatia ufaulu wa somo husika na ufaulu katika mwaka uliotangulia.
Kutokana na maelezo hayo, ni dhahiri kuwa zoezi la kupitia upya matokeo ya Kidato cha Nne 2012 litachukua muda mfupi na matokeo yatatangazwa hivi karibuni.

Selestine Gesimba
KAIMU KATIBU MKUU
WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI
10/05/2013
 
da afadhali ila mpaka sasa sijajua ni nani anatakiwa KUJIUZULU!!! teh teh yule katibu mkuu aliyepigiwa kelele na akina nanihii au this time atatakiwa AJIUZULU pamoja na waziri wake!!
 
Nyie hata mkitoa taarifa mbinguni bado hamtaeleweka hata huko.

Mnafanya upuuzi tu na elimu yetu.
 
Hii yote ni kucheza tu na vichwa vya watanzania, sijui tunamdanganya nani?
 
Kweli binadamu tumeumbwa tofauti. Mimi huwa nachukia kudanganywa, cha ajabu wengine wanathubutu hata kujidanganya wenyewe
 
ina maana Prof. Mukandala kakubaliana nao? Na Joyce je?
This country bwanaaaa.
 
Hivi Waziri wa Elimi bado hajajiuzulu tu? Udhaifu mkubwa sana katika elimu si matokea bali kianchosababisa kufeli kwa watoto na Wizara inajua fika chanzo!!!
 
vijana wengi wanaomaliza form 4 wengi wana umri wa miaka 18!! sasa kama hawa wakipigwa chini serikali itaonekaje?? na mwaka 2015 patakuaje?? hizi ni siasa tu hamna jipya...ila hapa tunaandaa bomu ambalo ni hatari zaidi ya la nyuklia!!! yetu macho..
 

Hivi mkandara hayupo jamvini?...
 
Serikali kuweni wawazi.
  • Utaratibu uliotumika mpya wa kupanga matokeo ni upi?
  • Utaratibu wa zamani ambao ndio sasa mnataka kuutumia ni upi?
 

Je wizara ina mpango gani kwa wale wahitimu wailio jinyonyonga kutokana na mipango yake mibovu?
 
Hizo zote ni namna 2, ili serikal isafishike. walipotangaza matokeo kwa nini hawakulichunguza hilo! waache kutudanganya watanzania, ninauhakika kabisa kama matokeo yatakuwa standerdized, matokeo ya kidato cha sita 2015 ziro zitakuwa kwa 75%, lasivyo wasithubutu uchakachuz huo, tafathar muwakataze!!
 
haya ni majanga tu.

Kwani izara wao hawakujua kama necta wamebadilisha grades mpaka inafika siku ya kuyangaza matokeo na wanayatoa bila wizara kujua na kwann wabadilishe bila kutoa taarifa kwa wadau wa elimu..?

Mpaka inafika kipndi sasa wanadhalilishana namna hii, sasa hatujui kama wanabadilisha matokeo kwa kumridhisha nani either wananchi au wao kwa wao, kwa kweli wameli koroga na sasa wanalinywa vizuuri kabisa hii ni historia mbaya kabisa, na mpaka sasa cjui ni mwananchi gani anayeweza kuwaamibi necta tena.

Manake wameshaonekana kama wachakachuaji.
 
Serikali kuweni wawazi.
  • Utaratibu uliotumika mpya wa kupanga matokeo ni upi?
  • Utaratibu wa zamani ambao ndio sasa mnataka kuutumia ni upi?
hayo ni maswali ya msingi ilipaswa watanzania tuambiwe,hawa watawala wanatudharau sana wananchi,hawatushirikishi ktk maamuzi ya msingi yanatugusa moja kwa moja katika maisha yetu!!inatia hasira sana.Mtu anatoa isiyo kuwa na data maana yake nini?taarifa kama vile amelewa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…