Taarifa kwa umma: Ufafanuzi wa taarifa iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kamera 40 kufungwa Kariakoo kwa Tsh milioni 514

Taarifa kwa umma: Ufafanuzi wa taarifa iliyosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu kamera 40 kufungwa Kariakoo kwa Tsh milioni 514

Joined
Jul 19, 2023
Posts
8
Reaction score
33
IMG-20250219-WA0002.jpg
IMG-20250219-WA0003.jpg
 
Hakuna hatua yoyote ya kuchukua hapo tuseme tu Asante kwa ufafanuzi ila me sioni tatizo..ni sawa na Mimi niseme billion moja kuleta maji wilayani..sio lazima mtoa taarifa aeleze kwamba mradi utahusisha survey sijui manunuzi n.k...processes sote tunajua
 
Kwanini msitoe ufafanuzi sahihi na wakueleweka tangu mwanzo wa utiwaji saini?
Lakini baadae mikshachafuliwa na watu wenye akili ndogo ndio mnatoka mashimoni na kuja kuleta ufafanuzi.
Nadhani hii tabia tuiache, taasisi zitoe na kuainisha kila kitu bayana na kwa ufasaha.
Lakini sio hii ya kutoa habari kisha kesho mnakuja kukanusha.
 
Usiri usiokuwa na ULAZIMA ndio chanzo cha matatizo yote haya, endapo kama taarifa za mchakato mzima wa mradi huo zingeweza kuwekwa hadharani tangu hatua za awali kabisa za mradi huo Basi taarifa za namna hii zisingeweza kujitokeza.

Najua ya kwamba Ofisi za Umma huwa mnaficha Sana taarifa za namna hii ili muweze kujitengenezea Mazingira mazuri zaidi ya kuweza kufanya Wizi, kula rushwa au kufanya Ufisadi bila kugundulika na umma. Uwazi huwa una kawaida ya kufichua Uovu na Waovu, Usiri usio na ULAZIMA huwa una kawaida ya kuficha Uovu na Waovu.
Baada ya kuona Wafichua Maovu (Whistle blower) wameanika hadharani uovu wenu mliouficha sasa mmeibuka haraka sana kutoka mafichoni ili kuja kujitetea hapa. Siku zote hizo mlikuwa wapi? Kwa Nini miradi ya umma Kama hii umma (Wananchi) ambao ndio walengwa Wakuu wa mradi huo mlikuwa hamuwapatii taarifa za muhimu kuhusu miradi yao?
 
Kwanini msitoe ufafanuzi sahihi na wakueleweka tangu mwanzo wa utiwaji saini?
Lakini baadae mikshachafuliwa na watu wenye akili ndogo ndio mnatoka mashimoni na kuja kuleta ufafanuzi.
Nadhani hii tabia tuiache, taasisi zitoe na kuainisha kila kitu bayana na kwa ufasaha.
Lakini sio hii ya kutoa habari kisha kesho mnakuja kukanusha.
Mimi nataka signed BOQ Tu iwekwe hapa inayoonyesha quantity ya camera
 
Mbona wadau akiwemo Mdakuzi wangu alitolea ufafanuzi mzuri tu? Hayo mambo ya kufunguliana kesi Mkurugenzi wa Jiji umefika mbali.

Taarifa hii rasmi ya ufafanuzi imetosha, na kupitia andiko la aliyeleta uzi wengi tumefahamu kuhusiana na ufungwaji huo wa kamera ambayo ni taarifa njema ya kupongezwa Mkurugenzi wa Jiji na watendaji wake.
 
Back
Top Bottom