Taarifa kwa wanaotaka Kusomea Kozi ya Maabara SUA, UDSM N.k

COARTEM

JF-Expert Member
Joined
Nov 26, 2013
Posts
3,603
Reaction score
3,658
1.Wataalamu wa Chuo Kikuu cha Sokoine, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kutoka Vyuo vingine vinavyofanana na hivyo, hawana sifa za kitaaluma za kuwawezesha kufanya kazi katika Maabara za Afya zinazohusika moja kwa moja na kumhudumia mgonjwa, yaani uchukuaji na upimaji wa vipimo vya mgonjwa.

2.Wataalamu wa Chuo Kikuu cha Sokoine, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kutoka vyuo vingine vinavyofanana na hivyo hawana sifa za kisheria za kuwawezesha kusajiliwa au kupata leseni chini ya Sheria ya Baraza la Wataalamu wa Maabara wa Afya nchini.

3.Wataalamu wa Chuo Kikuu cha Sokoine, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na kutoka Vyuo vingine vinavyofanana na hivyo, wana uwezo mkubwa wa kufanya utafiti wa kisayansi katika maeneo husika na hivyo kutoa majibu ambayo yatatumika kwa madhumuni ya kisayansi na siyo kushughulika moja kwa moja na mgonjwa

SOURCE:AJIRA ZA MAAFISA WATEKNOLOJIA WA AFYA (HEALTH LABORATORY SCIENTISTS)


 

Attachments

Jamaa wameshaanza kuondolewa kwenye ajira huko mahospitalini
 
Serikali inaanzosha kozi yenyewe

Mazao inayakataa.
 
Mmmhhh ilikuaje ikawaajiri?

Kwani hawa wateknolojia wa maabara wanaongelewa ni wale ambao hawakusoma vyuo vya afya km muhas..kcmc..bugando..nk.?? Bali walisoma mfano DIT (maana nako kuna kozi ya maabara.??).
 
1.Wataalamu wa Chuo Kikuu cha Sokoine, Chuo Kikuu ...

SOURCE:AJIRA ZA MAAFISA WATEKNOLOJIA WA AFYA (HEALTH LABORATORY SCIENTISTS)

Tangazo halina nembo ya wizara wala sahihi ya katibu mkuu wa wizara. Could it be a hoax?!?
 
kusoma maabara sio lazima ufanye maabara za hospitali
zipo maabara nyingi kama TBS,TFDA nk.

point hapa ni fupi kuwa wanaosomea hivo vyuo wana sifa za kufanya kazi maabara zote isipokuwa maabara za kitabibu.
 
Mnatubagua.basi kuna microbiology ya sua,ya udsm na ya muhas.semeni tumekosa medical ethics ambazo muhimbili ni somo la semista moja tu!mnajiona matawiiiii kumbe zero
 
Nakumbuka tulipokea wawili mwaka jana na tukasitisha ajira zao kwani hawa ni wale wa viwandani na sio kwenye vituo vya kutolea huduma za afya
 
Mh Kweli hawa wanasoma biotechnology yani wanadil na wanyama , mimea, viwanda. Shule yao haijakaa vizuri wanasomaga wakimaliza ndo wanapanguwa field kujifunza vipimo vya binadamu unakuta hawawezi kabisa yani wanafundishwaga na maatendant du . kozi imepinda haieleweki wanawadanganya na mikopo ya %100
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…