w0rM
Member
- May 3, 2011
- 81
- 192
Katika miaka ya hivi karibuni, Ulinzi wa Taarifa Binafsi ni muhimu sana maana taarifa za mtu zinaweza kutumika vibaya muda wowote bila ya muhusika kujua.
Leo nimewaza sana zile Hotel, Lodge, au Guest ambazo tunaenda na kuambiwa tuandike taarifa zetu kwenye daftari Mapokezi. Hivi zile taarifa huwa wanazilinda vipi na wanakaa nazo kwa muda gani? Unaweza kukuta tunajiuliza wale wezi wa "Tuma kwenye Namba hii" wanatoa wapi fedha kumbe wanatoa kwenye sehemu kama hizi.
Pale watu wanaacha namba za simu, majina halisi maana kuna sehemu wanataka kabisa utoe na kitambulisho cha NIDA. Hizi ni taarifa muhimu sana.
Ukiachana na hizi Lodge au Hotel pia kuna zile Ofisi huwa tunaingia na kutakiwa kuandika taarifa zetu hivyo hivyo kwa kweli najiuliza sana utunzaji wa taarifa zetu na matumizi yake baada ya hapo.
Swali jingine la kujiuliza ni kuwa daftari likijaa utunzaji wake unakuwaje? Je, wanafuata sheria inavyosema au inakuaje? Hili ni janga sana kwa kweli.
Mamlaka itusaidie kusimamia jambo na kuweka misingi muhimu.