Taarifa ya Jeshi la Polisi kutoka Mkoa wa Ruvuma

Taarifa ya Jeshi la Polisi kutoka Mkoa wa Ruvuma

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
3,984
Reaction score
13,760
WhatsApp Image 2024-10-04 at 17.37.58_f437c182.jpg

WhatsApp Image 2024-10-04 at 17.37.59_e649bebe.jpg

Hali ya ulinzi na usalama Mkoa wa Ruvuma ni shwari, na ushwari huu umetokana na ushirikiano mzuri uliopo baina ya Jeshi la Polisi na Wananchi kuhakikisha jamii na mkoa kwa ujumla unaendelea kuwa salama.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma linapenda kutoa taarifa ya mafanikio ya doria, misako, operesheni kwa kipindi cha mwezi Septemba hadi Oktoba, 2024 kama ifuatavyo;

Ni kwamba tarehe 03.10.2024 majira ya saa tano asubuhi huko maeneo ya Mtaa wa Sokoni, Kata ya Mjini Manispaa ya Songe na huko Kijiji cha Mtyangimbole Halmashauri ya Songea Vijijini tulifanikiwa kuwakamata wanawake watatu (3) waliofahamika kwa majina ya Anna Costa Mtete, Miaka 22, Mkazi wa Ndiwile Iringa, Grace Philipo Kihombo, Miaka 42, Mkazi wa Dar es Salaam, Adelaide John Kihaka, Miaka 62, Mkazi wa Dabaga Iringa, wakiwa na mali mbalimbali za wizi ambazo waliiba katika maduka tofauti tofauti yaliyopo Soko Kuu la Songea ambavyo ni, Vitenge 414, Kanga 6, Suruali Kadeti 31, Pasi za Umeme 2, Ndoo ndogo za Lita kumi za mafuta ya kupikia 10, Ndoo ya Lita Ishirini ya mafuta ya kupikia 1 pamoja na bidhaa mbalimbali za dukani wakizisafirisha kuelekea Mkoa wa Njombe kwa kutumia gari lenye namba za usajili T.576 EHV Toyota Hiace mali ya Rioba Mapunda wa Songea.

Jeshi la Polisi limefanya ufuatiliaji wa kina na kubaini mtandao wote unaojihusisha na matukio hayo ya wizi na kubaini kwamba watuhumiwa hawa wanatoka mikoa ya jirani na siyo Ruvuma, hivyo upelelezi ukikamilika watafikishwa mahakamani.


Pia kupitia Operesheni mbalimbali zinazoendelea kufanyika maeneo yote mkoani Ruvuma tumefanikiwa kukamata jumla ya kete 36 za bhangi na kuteketeza shamba la bhangi lenye ukubwa wa robo heka likiwa jumla ya miche 76 iliyolimwa kwa kuchanganywa na zao la mahindi.

Watuhumiwa wawili (02) wamekamatwa na wamefikishwa mahakamani kwa hatua za kisheria.

Kwa upande wa mafanikio ya kesi za mahakamani jumla ya watuhumiwa 05 wa kesi mbalimbali walifikishwa mahakamani na kuhukumiwa vifungo tofauti tofauti ambapo watuhumiwa wawili (02) wa makosa ya Kubaka walihukumiwa kifungo cha miaka 30 Jela kila mmoja, Mtuhumiwa mmoja wa kosa la kubaka alihukumiwa kifungo cha Maisha jela na Mtuhumiwa mmoja alihukumiwa kwenda jela miaka 13 kwa kosa la kupatikana na silaha.

Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma linatoa shukrani kwa wananchi na raia wema wa Ruvuma kwa kutoa ushirikiano na kuhakikisha kunakuwa na usalama na amani kwa kipindi chote cha ziara ya Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassani alipokuwepo mkoani Ruvuma.

Natoa wito kwa Wananchi wote wa Mkoa wa Ruvuma walioacha kutenda uhalifu kipindi chote cha ziara ya Mhe. Raisi waendelee kuachana na uhalifu kwani maisha yanaweza kuendelea bila kutenda uhalifu.

Imetolewa na:

Marco G. Chilya - SACP

Kamanda wa Polisi

Mkoa wa Ruvuma
 
Back
Top Bottom