Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
TARIFA YA KIFO
MOHAMED OMARI MKWAWA
MOHAMED OMARI MKWAWA
Mohamed Omari Mkwawa Akiwa Amekishika Kitabu: "Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru," kitabu kilichoandikwa na
Dr. Harith Ghassany
Mzee Mohamed Omari Mkwawa au kwa jina lingine Tindo alilopewa na Karume wakati wa harakati za ukombozi Zanzibar katika miaka ya 1950 amefariki dunia usiku wa Jumamosi kuamkia Jumapili tarehe 5 May 2015 nyumbani kwake Mwahako Tanga.
Marehemu anatarajiwa kuzikwa kesho Jumatatu Tanga mjini. Mzee Mkwawa alipata umaarufu mwaka 2010 baada ya kutoka kitabu cha Dr. Harith Ghassany, "Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru," kitabu kilichokuja kueleza historia ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa usahihi kuliko vitabu vyote vilivyopata kuandikwa kabla.
Ilikuwa Mzee Mkwawa ndiye aliyefichua siri kubwa iliyokuwa imefichwa kwa miaka mingi ya jeshi la askari mamluki wa Kimakonde waliochukuliwa kutoka mashamba ya mkonge ya Sakura wakapewa mafunzo katika mapori ya Kipumbwi na kuvushwa kwenda Zanzibar kusaidia mapinduzi ya tarehe 12 Januari 1964.
Mzee Mkwawa ndiye alikuwa akilivusha jeshi hili kwa majahazi kutokea Kipumbwi kwenda Zanzibar usiku wakiwa wamevaa mavazi kama wavuvi.
Mzee Mkwawa alikuwa na mchango mkubwa katika kutegua kitendawili cha mchango wa Tanganyika katika mapinduzi ya Zanzibar kiasi mwandishi Dr. Ghassany alipatapo kusema kuwa, "Ufunguo wa wa kitabu anao Mzee Mkwawa."
In Sha Allah taazia kamili ya marehemu ikieleza mchango wake katika historia ya Mapinduzi ya Zanzibar itafuatilia.
Inalilah Wainailaih Rajiuun