Taarifa ya kikao kifupi cha watumia bando

Taarifa ya kikao kifupi cha watumia bando

Ngaliwe

Senior Member
Joined
Dec 30, 2015
Posts
164
Reaction score
374
Kama mnavyojuwa gharama za vifurushi zimeongezeka maradufu kwa sisi watumaji na wasomaji wa taarifa mbalimbali za mitandaoni.

Hivyo tumekubaliana kwamba yoyote anataka kutuma video au audio yenye zaidi ya MB 2.5 atalazimika kuandika barua kwanza kwa admin na aeleze maudhui ya video yake au audio yake kabla ya kuileta groupn.

Pia kikao kimeshauri yoyoye mwenye video yenye zaidi ya MB 8 kabla ya kutuma awafahamishe Members wa group kwanza na awaelekeze nyumba anayoishi au atakapopatikana ili mwenye kuhitaji akodi bodaboda au Uber/ Bolt au Mwendokasi ili akufuate ulipo aje kuona hicho ulichonacho.

Mwisho kila Admin atakuwa na jukumu la kukaguwa wanaorudia rudia video kwa makusudi ili kuwafelisha wenzao kiuchumi.

Wako
Mwenyekiti wa Kikao
Mnyonge Mnyongeni

[emoji1431][emoji1431][emoji1431][emoji851][emoji851]
 
Ila kama video ya xx atume tu hivohivo hta kama una mb50 tutavumiliana tu
 
Je hakuna ukomo wa kutuma picha .?
Itapendeza kama group litapokea picha 3 tu kwa siku kwahiyo kabla yakutuma picha itakubidi uangalie kwanza kama nafasi ipo au imejaa ukikuta imejaa nivyema kuvuta subira hadi siku inayofuata na kama utajikuta kila uchwao unakuta kupo full nivyema ukaamka sa6 kamili usiku ili uwahi nafasi
 
Back
Top Bottom