Tumepotelewa na Mama anayeitwa Verediana Mataba au Mama Jane siku ya tarehe 27 Januari 2026 katika maeneo ya Kisesa Mwanza.
Mama huyu ni mwenyeji wa Buhare Musoma na alikwenda Mwanza kwa ajili ya matibabu ya kupoteza kumbukumbu. Anaongea lugha ya kiswahili na kikerewe kwa ufasaha.
Kwa mara ya mwisho alionekana majira ya saa 9 mchana maeneo ya Isangijo Kitongoji cha Mairinga kata ya Bukandwe akiwa amevaa nguo ya rangi ya njano na nyeusi kama inavyoonekana kwenye picha mojawapo.
Tunaomba kwa yeyote atakayemuona atoe taarifa kwa namba 0714500740
0769990721
Au kituo chochote cha Polisi.