Taarifa ya Miradi Mipya ya Idara ya Elimu Sekondari Katika Jimbo la Ngara

Taarifa ya Miradi Mipya ya Idara ya Elimu Sekondari Katika Jimbo la Ngara

Stephano Mgendanyi

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2020
Posts
2,833
Reaction score
1,301
Ndaisaba George Ruhoro Mbunge Wa Jimbo la Ngara Kwa kutambua na kuthamini mchango wa Elimu katika maendeleo ya Taifa ameendelea kupambana ili kuhakikisha mazingira ya Elimu kwa watoto wa kitanzania yanaendelea kuboreshwa na kuimalishwa zaidi .​

Kutokana na kero zinazopokelewa katika mikutano ya hadhara ya Mhe.Ruhoro nae kama mwakilishi wa wananchi amekuwa mstari wa mbele kufikisha Kero hizo kwa DR SAMIA SULUHU HASSAN Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Kwa mkutadha wa uboreshaji mazingira ya Elimu kwa ajili ya kujifunza na kujifunzia MAMA SAMIA SULUHU HASSAN ametoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa mabweni na nyumba ya mwalimu kama ilivyoainishwa.

1. Mabweni mawili Shule ya Sekondari Rusumo yenye thamani ya milioni 260

2. Mabweni mawili Shule ya Sekondari Muyenzi -Rulenge yenye thamani ya milioni 260

3. Mabweni mawili Shule ya Sekondari Lukole -Kasulo yenye thamani ya milioni 260

4. Nyumba ya mwalimu Shule ya Sekondari Murubanga -Nyamagoma yenye thamani ya milioni 100.

Ujenzi wa miundombinu hii itasaidia katika kupunguza adha za uhitaji uliopo katika Shule hizo na hivyo kutengeneza mazingira rafiki katika kuinua taaluma ya wanafunzi .

Wenu
Ernest RUHUGU
Katibu wa Mbunge

WhatsApp Image 2024-11-07 at 18.27.13.jpeg
 
Back
Top Bottom