Taarifa ya Msemaji Mkuu wa serikali kuhusu kimbunga Ialy na hali yake, Mei 19, 2024

Taarifa ya Msemaji Mkuu wa serikali kuhusu kimbunga Ialy na hali yake, Mei 19, 2024

Ojuolegbha

JF-Expert Member
Joined
Sep 6, 2020
Posts
1,278
Reaction score
797
Taarifa iliyotolewa na Msemaji Mkuu wa Serikali, Mobhare Matinyi leo Jumapili Mei 19, 2024 imesema kuwa TMA katika taarifa yake ya saa 12 jioni ya leo, imetabiri kimbunga hicho kilichopo umbali wa kilomita 680 kutoka pwani ya Tanzania, kuwa kitasababisha mvua kubwa na upepo mkali Jumanne.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa hali hiyo itasababisha upepo mkali baharini unaozidi kasi ya kilomita 40 kwa saa na mawimbi yanayozidi mita 2 hadi Jumanne, Mei 21 huku mvua kubwa ikitabiriwa kunyesha katika maeneo ya pwani ya nchi yetu kati ya Jumanne, tarehe 21 na Jumatano, tarehe 22 Mei, 2024

Taarifa hiyo pia imeshauri watumiaji wa bahari na wananchi kuchukua tahadhari na kufuatilia taarifa za utabiri wa hali ya hewa.

Kabla ya tishio hili la kimbunga Ialy, Mei 1, 2024, TMA ilitoa tahadhari ya kuwapo kwa kimbunga Hidaya ambacho baadaye kilikosa nguvu baada ya kuingia pwani ya Bahari ya Hindi na kusababisha madhara machache ikiwemo mvua kubwa ya upepo katika maeneo ya Mafia, Mtwara na Kilwa.

IMG-20240519-WA0073.jpg


PIA, SOMA:
-
TMA yatoa taarifa ya uwepo wa kimbunga Ialy Bahari ya Hindi
-TMA: Uwepo wa kimbunga “Hidaya” katika bahari ya Hindi Mashariki mwa Pwani ya Mtwara
 
Back
Top Bottom