Taarifa ya serikali kuhusu kiu

MKL

Senior Member
Joined
Mar 2, 2012
Posts
126
Reaction score
77
JAMHURI YAMUUNGANO WA TANZANIA
TUMEYA VYUO VIKUU TANZANIA
TAARIFA KWA UMMAKUHUSU MGOGORO WA WAFANYAKAZI NA WANAFUNZI KATIKA CHUO KIKUU KISHIRIKI DAR ESSALAAM CHACHUO KIKUU CHA KIMATAIFA CHA KAMPALA
1. Utangulizi
Kwa takribani wiki tatu sasa kumekuwa namvutano baina menejimenti kwa upande mmoja na wafanyakazi na wanafunzi kwaupande mwingine wa Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Kampala katika Chuo KikuuKishiriki cha Dar es salaam ama, kinavyojulikana kwa wengi, KIU. Mvutano huu ulisababishabaadhi ya waalimu kusitisha kufundisha na pia baadhi ya wanafunzi kujikutakatika mgomo hadi mvutano uliojitokeza utakapopatiwa ufumbuzi. Mvutano huuhatimaye ulisababisha Tume ya VyuoVikuu Tanzania kuingilia kati katika jitihadaza kuupatia ufumbuzi. Mnamo tarehe 14 Novemba 2012 Tume iliunda timu yawataalamu ambao walikwenda katika Chuo hicho na kufanya kazi kwa siku mbilikabla ya kuuanda ripoti yao. Ripoti ilibainisha maeneo mbalimbali yenyechangamoto ambazo budi zipate majibu. Ripoti hiyo ilijadiliwa katika kikao chaKamati ya Tume ya Ithibati na Chuo kupewa maelekezo katika maeneo mbalimbali napia kutakiwa kuleta majibu katika masuala yaliyoonekana kuwa na uhitaji wamajibu. Maelekezo haya yaliwasilishwa Chuoni kwa barua ya tarehe 4 Desemba 2012yenye kumbukumbu na TCU/A.40/69/Vol.IV/15 na kutakiwa kuleta majibu Tume kablaya tarehe 30 Desemba 2012. Kabla majibu hayajawasilishwa mgogoro wa wafanyakaziulianza na kufuatiwa na mgomo wa wanafunzi na hivyo tarehe 11 Desemba 2012Katibu Mtendaji wa Tume ya Vyuo Vikuu na Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Elimu yaJuu walikwenda katika Chuo hicho ili kuonana hususan na wanafunzi pamoja namenejimenti. Kimsingi, kikao kilihusisha menejimenti na wanafunzi kwa kuwasuala la wafanyakazi lilikuwa limeshapatiwa muafaka wa jinsi ya kulitatua.
Kufuatia mawasiliano ya awali baina yamenejimenti ya Chuo na viongozi wa wafanyakazi kuhusu mishahara ya wafanyakaziya mwezi wa Novemba 2012 pande zote zilikubaliana kwamba malipo hayo yaweyamefanyika ifikapo tarehe 14 Desemba 2012. Pia Chuo pamoja na waalimuwameafiki kufidia kipindi cha masomo ambacho kilipotea wakati wafanyakaziwanashughulikia mstakabali wa mishahara yao. Kufidia huko kutafanyika kati yatarehe 7 Januari na 11 Februari 2013 ili kutokuathiri mipango mengine yakimasomo ambayo tayari ilishapangwa kwa kipindi cha sasa hadi Januari 2013.Makubaliano haya yamewasilishwa TCU kwa barua ya Mkuu wa Chuo ya tarehe 10Desemba 2012 yenye kumbukumbu Na. KIU/PR/Vol.30/11/12. Tume imeelekezamakubaliano haya yatekelezwe bila kukosa ifikapo tarehe 14 Desemba 2012. Nimatumaini ya Tume kwamba hali hii haitajitokeza tena ili shughuli zaufundishaji katika Chuo hicho ziende kulingana na ratiba ya kila semesta.
Ifuatayo ni taarifa ya yaliyojiri katikakikao baina na menejimenti, wanafunzi, Katibu Mtendaji wa Tume na KaimuMkurugenzi wa Idara ya Elimu ya Juu.
2. Keroza wanafunzi dhidi ya Menejimenti
Kwa upande wa wanafunzi jumla ya kero 21ziliwasilishwa kimaandishi ili ziweze kupata ufumbuzi. Yafuatayo ni makubalianona maelekezo katika kero hizo katika makundi yafuatayo.
2.1. Ada namalipo mengine
Kumekuwa na hoja mbalimbali kuhusiana nakaro pamoja na malipo mengine katika programu mbalimbali. Hoja hizi zimejikitakatika ulipaji wa ada kwa dola za kimarekani na malipo mengine ambayomchanganuo wake hauko bayana kwa maana ya kuitwa “other charges”. Tume ilishatolea maelekezo suala la kulipa ada kwakutumia shilingi na siyo dola kwa Vyuo vyote kwa barua ya tarehe 15 Julai 2011yenye kumbukumbu na TCU.10.1/Vol.V/266. Chuo cha KIU kilikumbushwa suala hili kupitiabarua ya tarehe 16 Machi 2012 yenye kumbukumbu na. TCU/A.40/69/Vol.IV/8. Baadaya kutazama nyaraka mbalimbali zilizowasilishwa wanafunzi na menejimenti, Tumeimebaini kwamba wanafunzi waliojiunga mwaka huu wamepata barua za kujiunga na Chuoambazo zinaonyesha ada kwa fedha ya Tanzania isipokuwa kwa wanafunzi wanaotokanje ya Tanzania ambao ada zao zilionyeshwa kwa dola wakati walipojiunga na chuo.Wanafunzi hawa wako katika miaka tofauti ya masomo na wengine wanakaribiakumaliza. Kwa mantiki hii, malipo ya ada kwa wanafunzi hawa yatazingatiaviwango vilivyoonyeshwa wakati walipopata udahili. Nyongeza yoyote ya ada nilazima iwe imejadiliwa na kuidhinishwa na Tume kabla haijaanza kutumika. Na kwamantiki hii kiwango cha ada cha wanafunzi waliopata udahili wakati malipoyanafanyika kwa dola ya watalipa ada zao kulingana na kiwango cha ubadilishajiwa dola kwa wakati huo walipopata udahili na siyo vinginevyo.
Kwa upande wa suala la malipo mengineambayo hayakuwa na ufafanuzi wa kutosha, malipo hayo yamesitishwa hadiyatakapopatiwa muafaka. Tume imeelekeza menejimenti kulifanyia kazi suala hilikwa kina kwa kushirikiana na viongozi wa wanafunzi ambao nao wametoamapendekezo yao ya viwango katika maeneo mbalimbali.
2.2. Prospectus
Kukosekana kwa Prospectus katika chuolimekuwa ni suala amabalo wanafunzi wamekuwa wakiliwasilisha kwenye menejimentilakini ufumbuzi wake umeendelea kuwa kitendawili. Hali hii imesababisha wanafunzikulalamika rasmi na kudai haki yao ya kupata Prospectus. Suala hili lilikuwatayari limeshabainishwa na timu ya wataalamu iliyokwenda kukitembelea chuotarehe na hivyo Tume kwa barua yake yatarehe 4 Desemba 2012 ilikielekeza chuo kuwapatia wanafunzi Prospectus hiyo kablaya semesta hii kumalizika. Malekezo haya yanabakia palepale na pia chuokimelekezwa kuwapatia wanafunzi nakala ya Prospectus hiyo kwa mfumo wakielekroniki (e-copy) ifikapo tarehe 17 Desemba 2012 wakati uchapishaji wanakala za kutosha kwa wanafunzi na wafanyakazi ukiendelea.
2.3. Hudumaza Maktaba
Kumekuwa na malalamiko kuhusu utoshelevuwa vitabu na maandiko mengine katika maktaba ya chuo. Baada ya majadilianokatika kikao Tume imeelekeza menejimenti na serikali ya wanafunzi ipitie maeneombalimbali yanayolalamikiwa na kuandaa tarifa ya pamoja ya mapungufu yaliyopona mkakati wa kuyatatua. Taarifa hii iwe imekamilika ifikapo tarehe 28 Februari2013 na nakala yake kuwasilishwa Tume. Mapungufu yote ya maktaba yaweyamefanyiwa kazi na kutatuliwa kabla ya kufikia mwisho wa mwaka wa elimu wa2012/13. Serikali ya wanafunzi inatakiwa kulifuatilia kwa karibu suala hili nakutoa taarifa Tume endapo hakutakuwa na utekeleza kulingana na ratibailiyokubaliwa.
2.4. Hudumaza Intenet
Kumekuwa na malalamiko pia kuhusuupatikanaji wa huduma ya internet. Mada ya mjadala katika suala hili ilionekanani vyema menejimenti na viongozi wa wanafunzi wakaunda timu ya kulifuatilia kwaundani ili kugundua chanzo cha tatizo kwani Chuo tayari kilikuwa kimelipiahuduma hiyo kwa kampuni inayohusika na huduma hiyo lakini upatikanaje wakeumekuwa siyo wa kuridhisha. Chuo kimeanza mchakato wa kupata kampuni nyinginena pia kuangalia uwezekano wa kuunganishwa kwenye mkongo wa taifa. Timuitakayoundwa imeelekezwa kukamilisha kazi yake na kuwasilisha taarifa ifikapotarehe 1 Januari 2013
2.5. Mfumowa mitihani ya marudio
Wanafunzi pia walipendekeza kuwa na mfumowa supplementary examinations badalaya ule wa retake ambao unatumikasasa. Baada ya majadiliano ilibainika kwamba suala hili linahitaji utafitizaidi kabla ya kuamua kama mfumo wa sasa ubadilike. Hii inatokana na kukubalianakwamba kila mfumo una faida na hasara zake. Jambo la msingi ni kuhakikisha kilaupande, yaani wanafunzi, waalimu na menejimenti wanaelewa kwa ufanisi mfumounaotumika ikiwemo haki na majukumu yao katika utekelezaji wa mfumo huo. Chuokimeelekezwa kuwasilisha taratibu zinazotumika sasa katika mfumo wa retake ili Tume nayo iweze kungaliataratibu hizo na kutoa ushauri wake ikiwa itabidi kufanya hivyo katika hili.
2.6. Mfumowa utafiti na maandiko kwa wanafunzi wa mwaka wa tatu
Ilionekana pia kwamba wanafunzi hawanapicha kamili ya mfumo unaotumika katika masuala ya utafiti (research) namaandiko ya wanafunzi baada ya tafiti hizo. Kutokana na hali hii kujitokezaTume ilielekeza menejimenti ya Chuo itoe ufafanuzi wa kutosha kwa wanafunziwote kuhusu hili. Ufafanuzi huo uende sambamba na miongozo ambayo tayariimeshatolewa na tume kuhusiana na masuala ya mafunzo kwa vitendo katika ujumlawake. Kimsingi suala hili ni la utekelezaji wa mitaala iliyoidhinishwa kutumikakatika Chuo hicho. Ni vyema basi pande zote zikaelewa kinachotarajiwa namitaala hiyo na kukitekeleza huku miongozo mbalimbali iliyopo ikitiliwamaanani.
2.7. Sifaza waalimu
Wanafunzi pia wamehoji sifa za baadhi yawaalimu. Baada ya majadiliamo Tume imelekeza ukaguzi ufanyike na menejimentikuwasilisha Tume orodha na sifa za waalimu ambao wanafundisha masomo mbalimbalikwa hivi sasa. Orodha hii iandaliwe kwa kushirikisha viongozi wa wanafunzi nakitengo cha udhibiti wa ubora cha Chuo (KIUQuality Assurance Unit) na iwasilishwe Tume kabla ya tarehe 31 Desemba2012. Orodha hii iambtane na nakala za vyeti vya waalimu wote.
2.8. Serikaliya Wanafunzi na Katiba yake
Kutokana na majadiliano, imeonekanakwamba Serikali ya wanafunzi imekuwa haipati ushirikiano wa kutosha kutokamenejimenti. Pia serikali ya wanafunzi haina Katiba kama inavyoelekezwa naSheria ya Vyuo Vikuu (Sura ya 346 ya Sheria za Tanzania) na Kanuni za Serikaliza Wanafunzi za 2012 (GN.455/2012). Hili limekuwa sehemu ya mvutano baina yaserikali ya wanafunzi na menejimenti. Baada ya majadiliano, menejimentiimekubali kukaa na serikali ya wanafunzi na kukubaliana bajeti ya serikali yawanafunzi kulingana na viwango vinavyolipwa na wanafunzi kwa ajili ya shughulimbalimbali za wanafunzi. Pia menejimenti imekubali kuwasaidia wanafunzi nawafanyakazi kukamilisha Katiba zao ili kukidhi matakwa ya Sheria ya Vyuo Vikuukuhusu na masuala haya. Katiba hizi ziwe zimekamilishwa na kuwasilishwa Tumeifikapo tarehe 31 Januari 2013.
2.9. Uwakilishiwa wanafunzi kwenye kamati na vyombo mbalimbali vya Chuo
Ilibainika katika majadiliano kwambawanafunzi wamekuwa hawana uwakilishi wa kutosha katika baadhi ya kamati auvyombo vya Chuo ambavyo vinashughulikia masuala ya wanafunzi hususan yakitaaluma. Hali hii ni kinyume na matarajio ya Sheria ya Vyuo Vikuu. Tumeimeelekeza menejimenti ihakikishe wanafunzi wanapata uwakilishi katika kamatiau vyombo hivyo na kuwasilisha Tume taarifa ya utekelezaji wa suala hiliifikapo tarehe 31 Desemba 2012.
2.10.Ufundishajikatika shahada za udaktari wa binadamu na uhandisi
Wanafunzi pia wametoa malalamiko yaokuhusu utoshelevu wa mafunzo wanayopata katika masomo ya shahada za udaktari wabinadamu na uhandisi. Baada ya kupokea malalamiko hayo Tume itaunda timu yawataalamu itakayoshirikisha wataalamu wa TanganyikaMedical Association na EngineersRegistration Board ili kufanya uchunguzi wa kina kuhusu malalamikoyaliyojitokeza na kutoa mapendekezo yake. Zoezi hili linatakiwa likamilikeifikapo tarehe 15 Januari 2013 na hatua stahiki zianze kuchukuliwa baada yahapo. Sambamba na hili Tume inaandaa utaratibu wa kufanya tathmini ya masualambalimbali katika chuo hiki ili kujiridhisha kama masuala mbalimbaliyanatekelezwa kwa mujibu wa sheria.
2.11.Wanafunziwa kitanzania kufikiriwa kulipa ada ya chini kuliko wageni
Wanafunzi wa kitanzania walitoa ombi la kufikiriwakulipa ada ya chini kuliko wageni. Tume iliwaarifu wanafunzi kwamba hili nisuala la kisera na kwamba litafikishwa kwenye Bodi ya Wadhamini wa Chuo. Lakinipia wanafunzi walielezwa kuhusu mchakato unaoendelea katika Jumuia ya AfrikaMashariki kuhusiana na masuala ya ada hususan mapendekezo kwamba wanafunzi wanaotokanchi moja na kwenda kusoma nchi nyingine ndani ya jumua walipe viwango sawa nawazawa katika nchi hizo wanazokwenda kusoma. Pia serikali inafanyia kaziuandaaji wa mfumo wa kutambua ada ya mwanafunzi katika programu (studentunit cost). Kwa mantiki hii suala hili linahitaji kufanyiwa kazi zaidina vyombo vinavyohusika kabla ya muafaka kufikiwa na kutekelezwa.
2.12.Ratibaza vipindi pamoja na waalimu kuwa na vipindi vingi
Ilijitokeza pia kwamba baadhi ya vipindihususan vya masomo ya Kompyuta vimekuwa na ratiba isiyokidhi mahitaji nakusababisha wanafunzi kulundikana katika darasa moja wakati madarasa yapoambayo yangeweza kutumika katika masomo ya aina hiyo. Baada ya majadiliano Tumeimeelekeza suala hili liangaliwe na menejimenti kwa kushirikiana na uongozi wawanafunzi ili kulipatia ufumbuzi kabla ya semesta ya pili ya mwaka huu wamasomo kuanza mwezi Machi 2013.
2.13.Kitengocha Udhibiti wa Ubora cha Chuo (KIU Quality Assurance Unit)
Wanafunzi, pamoja na kupongeza uwepo waKitengo cha Udhibiti wa Ubora cha Chuo, wamelalamikia ufanisi wa kitengo hichona hivyo kupendekeza kiboreshwe zaidi ili kuweza kuleta tija iliyotarajiwa.Menejimenti pia imeridhia mapendekezo hayo na kuahidi kuyafanyia kazi kwa kushirikianana uongozi wa wanafunzi.
2.14.Mahafali
Kumetokea pia malalamiko kwa upande wawanafunzi wanaohitimu katika fani mbalimbali kulazimishwa kulipa kiasi chashilingi laki tatu na pia kutakiwa kwenda Uganda kwa ajili ya kushiriki katikamahafali. Suala hili lilikuwa katika masuala yaliyotolewa maelekezo natumekatika barua yake ya tarehe 4 Desemba 2012 yenye kumbukumbu na.TCU/A.40/69/Vol.IV/15 . Tume imetoa maelekezo kwa Chuo kwamba mwanafunzi anahaki ya kupewa cheti, stashahada au shahada husika endapo amehitimu na kufaulumasomo yake, halazimiki kushiriki katika mahafali na hivyo halazimiki kulipaada ya aina yoyote endapo hatashiriki katika mahafali hayo. Wakati kipindi chamahafali kitakapowadia, chuo kinawajibika kutoa tangazo la kuwataarifu wanafunzikuhusu mahafali hayo na wale watakaopenda kushiriki wanahiyari ya kufanya hivyona kulipia ada ya majoho ambayo itapangwa na chuo. Pia chuo kimeelekezwakuandaa utaratibu wa kufanya mahafali yake hapa Tanzania kuanzia mahafali yawanafunzi watakaomaliza masomo yao katika mwaka wa masomo wa 2012/13. Mahafalihayo yataongozwa na taratibu za mahafali zinaotumika hapa nchini.
2.15.Mihadharaya kielimu
Pia yalitolewa malalamiko ya wanafunzikuhusu kufutwa kwa mihadhara katika semesta ya kwanza. Menejimenti ilielezatatizo lililojitokeza hadi kusitisha mihadha na kuahidi kurudisha mihadharahiyo kuanzia Januari 2013.
2.16.Matokeokutolewa kwa wakati kupitia mtandao.
Wanafunzi pia walilitoa malalamiko yaokuhusu kucheleweshewa matokeo yao. Pia wakati mwingine matokeo halisi yawanafunzi yamekuwa na utata. Kutokana na hali hii pande zote zilikubalianakutoa matokeo kwa njia ya mtandao. Zoezi hili liwe limekamilika na mfumo kuanzakutumika katika semesta ya pili ya mwaka wa masomo wa 2012/13.
2.17.Utaratibuwa Wanafunzi wenye sifa za Diploma Kujiunga na Kozi mbalimbali za ngazi yaShahada
Suala hili lilijadiliwa na kufikiamuafaka kwamba taratibu zilizoainishwa katika miongozo ya Tume na ile ya Barazala Elimu ya Ufundi (NACTE) zitumike. Mwanafunzi mwenye diploma inayotambuka naTume au NACTE anaweza kujiunga na elimu ya juu ngazi ya Shahada kama ana sifastahiki. Matokeo ya wanafunzi wote wenye Diploma sharti yawe yamewasilisha Tumeau NACTE kwa wakati na kuingizwa kwenye mtandao (database) ambayo iko ilimwanafunzi husika aweze kuomba udahili kupitia CAS. Menejimenti pamoja naviongozi wa wanafunzi wamaekubaliana kulifanyia kazi hili kabla ya kuifikamwisho wa mwaka wa masomo wa 2012/13.
2.18.Malipowakati wa kujiandikisha chuoni
Wanafunzi walitoa malalamiko yao kuhusuchuo kuwatoza ada wakati wa kujiandikisha (registration fee) na kwamba hililisifanyike kwa sababu baadhi yao tayari walishalipa ada ya udahili kupitiaCAS. Ufafanuzi ulitolewa kwamba ada ya udahili kupitia CAS ni tofauti na ada yausajili chuoni na hivyo wanafunzi wanawajibika kulipa kulingana na viwangovilivyoidhinishwa na mamlaka za chuo.
3. Hitimisho
Kutokana na kikao hiki Tume imebaini piamapungufu katika mawasiliano baina ya wanafunzi, wafanyakazi na menejimentihali ambayo imepelekea kwa pande husika kutoaminiana. Tume na Wizara zinashauripande zote kuwa na mawasiliano yenye nia ya kutatua matatizo badala ya kuyaleana hivyo kuwa tatizo kubwa mbele ya safari. Hali kadhalika Tume imebainimapungufu ya jinsi masuala mbalimbali yanavyoshughulikiwa hususan kukosekanakwa kumbukumbu za kimaandishi kuhusiana na changamoto mbalimbali zinazojitokezaChuoni na jinsi zinavyoshughulikiwa na pande zinazohusika. Kumbukumbu hizi huwazinasaidia katika kijua kiini cha tatizo, jinsi lilivyoshughulikiwa,yaliyojitokeza na ni msaada wa aina gani unaweza kupatikana kutoka sehemunyingine nje au ndani ya Chuo chenyewe. Ni vyema pande zote zikakumbuka kwamba“Chuo” ni vitu vingi vinavyofanya kazi kwa pamoja ikiwemo wamiliki, menejimenti,wafanyakazi na wanafunzi. Tume inashauri pande zote kufanya kazi zake kwakaribu na kuweka kumbukumbu za kimaandishi katika masuala mbalimbali.
Kikao pia kilibaini haja ya kuwa namabadiliko katika mitizamo. Baadhi ya wanafunzi na wafanyakazi wanaamini kwambaTume au Wizara ni lazima ifike Chuoni na kutatua matatizo yaliyopo hapo Chuoni (micro management). Kila Chuo kina vyombombalimbali vya kutatua changamoto mbalimbali kwa mujibu wa Sheria ya Vyuo Vikuu.Tume inapenda kuwaasa wananafunzi, wafanyakazi na menejimenti kufuata taratibuzilizopo ndani ya Chuo ili kutatua matatizo mbalimbali yanayojitokeza. Tume piainashauri wadau wa elimu kuisoma kwa umakini Sheria ya Vyuo Vikuu ili kujuanamna ya kutatua changamoto mbalimbali za elimu ya juu Vyuoni. Hili litasaidiasana katika kupata ufumbuzi wa changamoto mbalimbali kwa wakati na kablahazijawa kero.
Mwisho Tume inapenda kutoa wito kwawanafunzi, wafanyakazi na menejimenti ya Chuo na Vyuo vingine nchini kuchukuahatua kurekebisha kasoro mbalimbali zinazojitokeza Vyuoni kwa wakati kablamadhara makubwa hayajajitokeza. Kinga ni bora kuliko tiba.
Imetolewana
KatibuMtendaji,
Tumeya Vyuo Vikuu Tanzania,
S.L.P.6562, DAR ES SALAAM
Email:es@tcu.go.tz
Simu:+255 (0) 22 2772657









 
Sina hakika hapo kwenye red kama kunaweza kutatuliwa. Na sababu ni hizi:-
1. Chuo kinaweza kutoa option, ada ni Dola 650 kwa Semister/mwaka au Tsh. 1,137,500/ per semister au mwaka. Hii ada ya sh. 1137,500 ni Dola iliyobadilishwa kwa exchange rate ya 1750 (650x1750=1,137,500). Ukiwa na Cash ya 1,137,500 na kuamua kuibadilidha katika dola kwa sasa ni (1137,500/1605=USD 708; USD 58 extra. Hivyo mathematician ataona bora alibe kwa dola kwa kuwa rate yao iko fixed katika specific figure amabyo ni kubwa kuliko. Ni bora muwaambie watumie ex. change halisi za BOT badala kila mmoja kujiwekea kivyake
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…