comte
JF-Expert Member
- Dec 11, 2011
- 9,019
- 6,825
Nimeikuta mahali kutoka kwa mwananchi wa kawaida kutoka kijijini kwetu, amezungumza haya kama maoni yake binafsi:
"Taarifa ya utafiti wa uviko -19(covid -19) inatoa mapendekezo zaidi na sio hali ya sasa ya corona nchini, na hali ya corona kwa siku zilizopita na athari zake.
Binafsi nashangaa sana Profesa kutoa taarifa dhaifu kiasi hicho kama mtu asiye na utaalamu wa masuala ya utafiti.
01. Taarifa haijaeleza hali ya Corona kwa sasa nchini. Hii ingetusaidia kujua tupo katika hatari kiasi gani. Lakini wao hawakufanya hivyo.
02. Tulitarajia kuona taarifa ikifafanua kwa kina madhara makubwa ya kiafya yaliyotokana na Corona katika taifa letu kwa kushindwa kufuata njia za kitaalamu kwa muda mrefu. Lakini hamkufanya hivyo.
03. Taarifa ingeeleza, namna mlivyofanya utafiti kwa kuchukua baadhi ya waathirika wa Corona waliopona na ambao bado wanaumwa na kuwafanyia utafiti kisha kuja na majibu ya utafiti huo.
04. Na kwakuwa tayari watu walikuwa wanatumia nyungu(kujifukiza). Ninyi mngetoa sababu za utafiti wenu kwanini watu wasitumie nyungu, na madhara ya nyungu hizo kisayansi ili kuwakinga wasiendelee maana huenda hazisaidii. Hakuna utafiti wa kitaalamu unaofanyika duniani bila kuanza na njia ambazo jamii husika ilikuwa ikizitumia. Na hii ni njia bora ya kuwatoa watu katika imani ya nyungu waliyokuwa nayo na kuwapeleka kwenye njia sahihi, bila kufanya hivyo bado hujaisaidia jamii husika.
05. Taarifa ingeeleza namna walivyozifanyia tafiti chanjo zinazosemekana kuzuia corona hata wakati wa taarifa hiyo wangezitolea ufafanuzi. Wanasema kuruhusu chanjo. Je, Wamefanya utafiti gani wa kutushauri tutumie chanjo? Au wamekopi taarifa za watu wengine? Badala ya kuja na majibu chanjo ipi itumike kwa ajili ya watanzania, wao wanakuja na mapendekezo mengine kabisa, inamaana hata chanjo hizo hawajazifanyia utafiti.
Leo ukiwauliza chanjo ipi sasa tutumie? Wanayo majibu hapo? Kitaalamu hakuna chanjo mpaka sasa inayoweza kuzuia corona. Sasa kama maprofesa hao wangekuja na majibu pia athali zitokanazo na chanjo hizo na sio kusema chanjo iruhusiwe pasipo kutoa athali zitakazotokea moja kwa moja au kwa kizazi kijacho. Huo ni udhaifu mkubwa sana wa kamati hiyo. Sasa ni nan atakayetupatia majibu ya chanjo ipi itumike kama kamati yenyewe imeshindwa? Au ndio tusubiri wanasiasa watuchagulie? Au tunafuata kile mataifa mengine na who yatakavyosema?
Basi tu, ila mnaudhi sana mpaka tunashindwa kuelewa tuna viongozi wa namna gani. Hii nchi ni kupokezana tu, leo kwenu kesho kwetu.
Kazaneni sana na maamuzi hayo. Kama makusayo ya mapato kwa mwezi yameshuka, ni vyema mkakazana hata kukusanya kodi kwa nguvu kuliko kujipendekeza kiasi hicho ili tupate pesa za bure kutusogeza mbele.
Mithali 26:28 "Ulimi unenao uongo huwachukia wale uliowajeruhi, na kinywa cha kujipendekeza hutenda uharibifu "
Kama kweli chanjo hizo zingekuwa zinafanya kazi, kwann watuzuie kwenda huko kwao kama kweli wana kinga.
Kama kweli una ulinzi, kwanini uogope mwizi?
Wao wazungu wamechanjwa, kwanini waogope waafrika kwenda kwao kama kweli chanjo zinafanya kazi?
Mali zipo Afrika, hata mngejikausha wangewatafuta tu.
Niwatakie majukumu mema lakini
Mithali 27:1 "Usijisifu kwa ajili ya kesho, kwa maana hujui yatakayozaliwa na siku moja"