Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 53,857
- 121,995
Ile Ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa hesabu za serikali, CAG, Ludovic Utouh, ijulikanayo kwa jina maarufu la Ripoti ya Ukaguzi, itawasilishwa rasmi Bungeni mjini Dodoma siku ya Jumanne Ijayo, Tarehe 20 April, 2010 Saa 3:05 asubuhi.
Baada ya kuwasilishwa mezani kwa ripoti hiyo, CAG, Ludovick Utouh atafanya mkutano na Waandishi wa habari ambapo atatoa mhutaasari wa ripoti hiyo, itakayofuatiwa na maoni ya Wenyeviti wa Kamati za Hesabu za Serikali (John Cheyo), Serikali Mitaa (Dr. Wilbroad Slaa na Mashirika ya Umma (Zitto Kabwe) kwenye ukumbi wa Press Conference wa Bunge.
Kuwasilishwa kwa ripoti hiyo kunaifanya ripoti hiyo kuwa public document, hali inayopelekea wanahabari kuipongeza serikali maeneo iliyofanya vizuri, na kuitundika msalabani maeneo yenye maroroso.
Kama kawaida ya habari, serikali ikifanya vizuri sio habari kwa sababu ndio inavyotarajiwa kufanya vizuri, habari kubwa ni pale inapoboronga.
Ripoti ya Mwaka huu pia itatoa picha halisi ya mrejesho wa matumizi ya lile fungu la fedha za EPA, zilizorudishwa, hivyo kumaliza minong'ono kama kweli zilirudi ama kilikuwa ni kiini macho tuu.
Uthibitisho wangu kuwa fedha ni kweli zilirudi, ni kwa baadhi tuu ya washtakiwa kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria, hawa ni wale waliogoma kurudisha. Ila hata hao waliofikishwa mahakamani kama kina Jeethu (Jitu) Patel, wamefikishwa kwa kudaiwa kiasi kidogo tuu kile ambacho hawakukiridisha, hii ikimaanisha kile kiasi walichorudisha, hawajashitakiwa nacho.
Ripoti ya mwaka huu pia itakuwa ya kwanza kuainisha balozi moja moja sio kama ile inaoziweka balozi zote ndani ya kapu la Wizara ya Mambo ya Nje, hali itakayopelekea uwezekano wa Wizara kama Wizara, kupata hati safi licha ya uchafu wa kwenye baadhi ya balozi zetu.
Angalizo, Ripoti ya ukaguzi, ni ile ripoti inayaangalia kama sheria, taratibu na kanuni za matumizi ya fedha za umma zimefuatwa na sio ripoti ya ufanisi (efficiecy) au thamani, (Value for Money). Kwa maneno mengine, kama imepitishwa ndizi moja yakisukari ni Sh. 10,000, bajeti ya ndizo hiyo ilipitishwa, taratibu ya kuinunua ndizi hiyo zilifutwa, then ripoti ya ugaguzi huo, itakuwa niripoti safi.
Tuisubirie Jumanne hiyo kama kawaida yetu, JF ni wa kwanza kupata habari, naahidi pia kuwa tutakuwa wa kwanza kuipata na kuirusha.