Taarifa za kikachero za Special Branch 1950s

Hapa umetudanganya...Abdul Sykes alikuwa mfanyabiashara sokoni kariakoo kipindi cha kudai uhuru....
 
Hapa umetudanganya...Abdul Sykes alikuwa mfanyabiashara sokoni kariakoo kipindi cha kudai uhuru....
Laki...
Sina sababu ya kusema uongo.

Abdul Sykes alikuwa Market Master Kariakoo Market nafasi ambayo ilkuwa ameshika Mwingereza Brian Hodges.

Mkusanya Ushuru (Collector) alikuwa Shariff Abdallah Omar Attas katika watu wa mwanzo kujuana na Nyerere na mkewe Bi. Chiku bint Said Kisusa ndiye yuko kwenye picha anamsindkiza Nyerere Uwanja wa Ndege safari ya kwanza UNO 1955.


Shariff Abdallah Attas kama alivyokuwa katika 1950s.

View attachment 2226316
Kulia wa kwanza ni Bi. Chiku bint Said Kisusa mke wa Sharif Abdallah Attas akimsindikiza Nyerere Uwanja wa Ndege Dar es Salaam safari ya kwanza UNO 1955.
 
Labda tuanzie hapa.
Waliofuta historia halisi ya TANU ni akina nani, lini, wapi, kwanini?
Zanzibar...
Inatosha kwa mtu kusoma kitabu cha Historia ya TANU Cha Chuo Cha CCM Kivukoni (1981) ukaona jinsi historia yake ilivyo tofauti na histora hii unayosoma kutoka kwangu kwa ushahidi wa nyaraka na picha.

Ukithibitisha ukwel huu unakuwa jibu ushalipata.
 
Hiyo picha ya Nyerere mbona sioni mabegi hapo? Halafu iweje asindikizwe na wanawake, Badala ya viongozi wenzake wa TANU..?.. Ungesema labda hapo alikutana na wanawake wa TANU wakapiga picha ya ukumbusho ungeeleweka..Historia yako bado ina walakini.
 
Hiyo picha ya Nyerere mbona sioni mabegi hapo? Halafu iweje asindikizwe na wanawake, Badala ya viongozi wenzake wa TANU..?.. Ungesema labda hapo alikutana na wanawake wa TANU wakapiga picha ya ukumbusho ungeeleweka..Historia yako bado ina walakini.
Laki...
Picha inazungumza maneno 1000.
Angalia picha hiyo hapo chini:

 
History is not about the past events... it's about selected event...
 
Mzee nakuona unavyopata tabu sana na Nyerere kuimbwa kila kona ya dunia. Nakuona unavyotamani baba yako ndio awe badala ya Nyerere. Umechelewa sana. Hiyo Historia huwezi kuibadiri sasa. Kuna muda nakuonea huruma sana
 
Mzee nakuona unavyopata tabu sana na Nyerere kuimbwa kila kona ya dunia. Nakuona unavyotamani baba yako ndio awe badala ya Nyerere. Umechelewa sana. Hiyo Historia huwezi kuibadiri sasa. Kuna muda nakuonea huruma sana
Sweet...
Hapana sioni tabu wala sina tatizo na Mwalimu katika umaarufu wake ambao anastahili.
Wala sikuandika kitabu cha Abdul Sykes kwa kutaka ashindanishwe na Nyerere.

Nngefanya hivyo kitabu changu kingekufa siku nyingi.

Naamin hata wewe ukiwa umesoma historia ya TANU kama klivyoandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni na ukasoma kitabu cha Abdul Sykes utaona kuwa vimepishana sana katika ukweli.

Huu ukweli ndiyo nguvu yangu na ndiyo umekifanya kitabu cha Abdul Sykes kipendeke.
Sijachelewa.

Sasa kitabu kinakwenda toleo la tano toka kichapwe kwa mara ya kwanza na Minerva Press, London 1998.

Wakuonewa huruma ni wewe ambae umekuja kujua kuwa historia uliyokuwa ukisomeshwa toka haikuwa historia ya kweli.

Leo wewe uko hapa mimi nakusomesha historia ya kweli si ya TANU peke yake bali historia ya Mwalimu Nyerere mwenyewe.

Naamini kabisa kuwa yote unayosoma kwangu hukupata kuyasoma popote.

 
Historia yako tulio wengi hapa jf tumeielewa na nadhani toka umeanza kuisimulia na kuiandikia vitabu itakuwa imeshakumbukwa kwa kifupi haitafutika tena maana umeiweka katika maandishi...tatizo lipo katika kurudia rudia na kublame kila mda as ifu kuna kitu unakitafuta kama fidia kwa hao wazee wako walipigania Uhuru
 
Sajo...
Uandishi wa mitandaoni ni tofauti na mawasiliano ya uso kwa uso.

Katika mitandao kila siku kila saa na kila nukta wanaingia watu wapya ambao ndiyo siku ile ananisoma mimi na anapata uelewa wa somo ninalosomesha.

Katika mitandao lazima mwalimu arudierudie.
Haiepukiki.

Mimi hapa nipo nasomesha na narudia masomo yangu kwa wanafunzi wapya.
Kumbukumbu zangu mathalan zinanambia wewe ndiyo kwanza tunaonana hapa barzani.

Sasa ikiwa wewe ushanisoma sana huna tena haja ya kurejea kunisoma unapita tu bandiko langu unasoma viti vingine.

Jambo jepesi kabisa wala huna haja ya kuniandikia na kulalamika.
Sidhani kama kusahihisha historia iliyokosewa ni kulaumu.
 
Umeeleweka Ulamaa,endelea kumwaga madin .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…