Asante sana kwa information mkuu. Ila nina swali moja nataka kuuliza, je kama ninahitaji mkopo wa kuanzisha biashara na sina kiwanja, nyumba wala shamba ninafanyaje? na ni benk gani ambayo itanifaa??
Asante sana kwa information mkuu. Ila nina swali moja nataka kuuliza, je kama ninahitaji mkopo wa kuanzisha biashara na sina kiwanja, nyumba wala shamba ninafanyaje? na ni benk gani ambayo itanifaa??
sidhani kwanba hizo data zako ziko sawa , na kushangaza hiyo TIB unasema ni 5%, tanzania hakuna benki itakayokupa chini ya riba asilimia 10 na hii ukikopa kwa USD , kwa Tsh mkopo unakwenda kwa riba ya aslimia 14 , CRDB, NMB , EXIM , NBC
"kuanzisha biashara" - hapa ndipo changamoto ilipo kwenye mabenki na taasisi zetu za fedha, sidhani kama wanatoa hata kama unayo security, kama kuna mdau anayejua atujuze tafadhali
mfano, ninataka kununua scania truck na security ninayo? benki gani inaweza kukupa facility hii?
Ukiwa na security + business plan benki nyingi zitakupa mkopo endapo zitaona bila shaka yoyote kwamba utaweza kuurudisha!
thread yako ni zaidi ya lecture, pia ni data bank ya mambo muhimu yanayohusu mikopo
ninauhakika wengi watajifunza na kunufaika
Ahsante sana kaka,
Nimeomba kwa mods waiweke kwenye sticky thread ili watu wengi waweze kuitembelea. Nitajitahidi kufanya marekebisho kadri ninavyopata taarifa sahihi.
Kuna watu wamelaumu kwamba baadhi ya taarifa siyo sahihi..Hii tabia inasikitisha kwani wao wengetusaidia kurekebisha pale ambapo tumekosea ili kila kitu kiwe na usahihi wa kutosha.
Inshallah tuendelee kusaidia ili mwisho wa siku tuondoe ila dhana kwamba Watanzania tunalalamika sana ila tunatenda less hata pale tunapopewa nafasi.
DC
Equity bank ya wakenya nasikia inatoa mikopo pasipo na magumashi na interest zao zipo chini sana. Kwasasa wameshafungua matawi tz dar, mwanza, arusha. All the best
Kama una taarifa sahihi tupatie mkuu...Hizo ndio zililetwa na mdau mmoja!
2. FINCA .....Nimepata taarifa kuwa mtu akikopa 15mil anatakiwa kurudisha 1.7mil kwa mwezi ambayo inatupa interest ya 33.3%
Mwenye taarifa zaidi atuwekee hapa ili tuweza ku-update hii page ili iwasadie wale wanaohitaji mikopo ili wajikwamue!
Babu DC!![/COLOR]
khs FINCA ninavyofaham;
Unaweza kopa kuanzia 500,000 mpaka 15m kwa mkopo wa mtu binafsi(masharti uwe na biashara yenye mzunguko ndani ya mwezi mmoja ili uweze kufanya rejesho la principal na interest) hawahitaji uwe na account na kama documentation itaenda vizuri unaweza pata mkopo ndani ya siku 7. Interest yao ni 3 percent ya loan kwa mwezi. Na term zao zinaanzia mpaka miezi 3 hadi 18, that means depending with the loan term its where the final interest is determine. Kama miezi 6 basi interest ni 18percent. Hawana overdarft coz ndio kwanza wanajipanga waanze huduma ya savings this year. Nawakilisha.
Najua fika kama ulivyoeleza anayeanzisha biashara huwa amefanya tathmini ya kutosha na kujiridhisha kwamba atapata faida na biashara itasimama.
Hata hivyo si hakika kama mafanikio yatafikiwa kama business plan ilivyo, maana kuna mengi yanahitajika kuweka sawa ili biashara isimame na enzi hizi za ushindani wa kibiashara na ubora wa bidhaa na huduma. Na hadi biashara isimame kwa haraka ni miezi 6 na pengine huchukua hadi miaka miwili.
Kiwango cha riba bila uficho kiko juu mno na kabisa kwa nchi maskini kama Tanzania. Nashangaa nchi tajiri riba inazidi kuwa chini kila kuikicha wakati nchi maskini ndio wanapandisha riba kama hawatumii akili vile.
Mikopo mingi ya bongo ni kati ya mwaka mmoja na miaka mitano, lakini riba ni juu sana kana kwamba ni mkopo wa miaka zaidi ya 30. Riba ingekuwa walao 12% ingekuwa fair hata hivyo ni bado juu kutosha lakini hii mnayotaja inatisha. Utakachochuma unachumia bank tu usipokuwa mwangalifu hata mtaji utaishia kwao.
Wana dirisha maalum la kilimo ambalo linatumia pesa ya ruzuku ya serikali na riba yake ni 5% na kuna mikopo ya biashara nyingine zote ambazo riba yake ni negotiable kuanzia 8% hadi 15%
Nina brochure zao ntascan nijaribu kuattach km zitasaidia hapa. Mimi nilipeleka business plan nikijaribu kupata response kuhusu expansion ninayotarajia kufanya 2013 waliposoma wakaniambia watanipa na wakaniomba wanipe sasa hivi twice ili nifanye two projects at once nyingine nifanye magharibi inayofanana na hiyo baada ya kuridhika na plan
Unaweza kutusaidia kufuatilia na kutupa uhakika?
DC