Taasisi gani wanakopesha kwa riba nafuu?

kirisha

JF-Expert Member
Joined
Feb 24, 2017
Posts
573
Reaction score
663
Wakuu mimi ni kijana mjasirimali

Nimepambana kwa muda hatimaye nimepata kaduka kangu kapo mjini kati

Sasa kulingana na pesa zangu za kuungaunga nimeshindwa kujaza mzigo nipige pesa

Nilikuwa naomba mnisaidie ni wapi naweza kupata mkopo wa milioni 2 wa riba nafuu kwa mwanza mjini ili niweke mzigo nipige show

Au mnanishauri aje ndugu zangu
 
Tupe details za hilo duka. Je ukipewa hiyo 2mil utarudisha kiasi gani?
 
Anaposema nafuu unaongelea riba ya kiasi gani kwa mwezi au mwaka
 
Kiukweli hakuna. Wote riba zao zitakuwa zimechangamka, kwa lengo la kupata faida nono. Hivyo jitahidi uende tu mdogo mdogo kupitia huo mzigo ulio nao.
Mzigo niliyonao umeshuka sana yani Kama nimefika mwisho vile
 
Nyamhanga maiklofinensi
Maboto maiklofinensi
Chogo maiklofinensi
Tuone maiklofinensi
Ndaki maiklofinensi
Ndulu maiklofinensi
Hizi wamegoma kunipa milioni 2 wanataka wanipe moja na nikiangalia moja siwezi kufika popote
 
Mcheki kilyeson microfinance, Kwa mkopo wa haraka wenye riba nafuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…