Pembejeo za kilimo kama vile trekta na mashine za kusaga, kukoboa, kukausha nafaka na kukamua mafuta na vitu vingine bado upatikanaji wake kwa wakulima umekuwa ni kitendawili mfano wakulima wamekuwa wakinunua mashine za kukamua zabibu kutoka china lakini wamekuwa wakilalamika zinakufa haraka baadae taasisi kama temdo (Tanzania engineering, manufacturing and design organization) ilifanya utafiti na kugundua kwamba chuma kulichotumika ni aina ya kasti kina vunjika kwa haraka na mbadala wake wakaweka chuma cha stili lakini mashine iliuzwa bei ghali zaidi ya ile waliyonunua China kama mara mbili yake mpaka kufanya wakulima wengi kushindwa kumudu hiyo bei.
Lengo kuu la hizo taasisi ni kumkwamua mkulima kwa kumwezesha kumudu na kupata pembejeo za kilimo kwa urahisi zitakazo msaidia kufanya kilimo chenye tija kitakacho mkwamua yeye na familia yake na kuchangia pato la nchi lakini badala yake sido na hizo taasisi nyingine zinazofanya tafiti zimeishia kwenye tafiti tu na hata wakija kutengeneza zinakuwa za maonesho tu ya saba saba na nane name mfano kama zile parachichi walizo lima kule mbeya nyingi zinaoza na watu walikopa wakaweka hela maana serikali iliwaambia walime baadae wakakosa soko yuko tu mwekezaji mmoja ambaye ananunua kwa bei ya chini sana mfano gunia moja ananunua kwa shilingi 15000-20000 wakati yule akikamua mafuta yake chupa ya lita moja anauza kwa shilingi 30000
Hii taasisi ya serikali kama TIRDO (Tanzania industrial research and development organisation) ilifika pale kwa ajili ya maonesho ya nane nane na kuja na mashine ndogo ya kutoka nchi za nje kuwaonesha jinsi wale wakulima wanavyoweza wakafaidika na hiyo mashine ambayo wataweza kukamua wao wenyewe moja kwa moja na kisha kutafutiwa soko ili kuweza kuuza hayo mafuta yao lakini mara nyingi yale maonesho ya hizo mashine huishia hapo na hata wakija kutengeneza huuza kwa bei ghali ambayo ni ngumu kwa mkulima wa kawaida kuweza kumudu gharama za kuinunua.
Nilikuwa nashauri kwa mfumo huu ni ngumu kumwokoa mkulima wa kawaida katika hii hali nilikuwa nashauri serikali ifanye mpango maalam kwamba wakulima wakopeshwe hizo mashine alafu wawasajili waendelee kurejesha kidogo kidogo tukifanya hivyo tutainua wakulima wengi sana na kuwatoa katika hali ya umaskini na utegemezi, na tutazisaidia kukuza soko kwa hizi taasisi maana zitazalisha mashine nyingi na kuziuza kuliko kuzalisha chache alafu kukosa soko kutokana na bei yake kuwa juu.
Ukiangalia kama mabaki ya matunda kama vile ganda la machugwa hutumika kutengeza malighafi ambayo inauzwa ghali ambayo ipo pale TIRDO mfano tukiwaweka watu kwenye vikundi na kuwapa hizi mashine na mafunzo namna ya kutengeneza tungeinua watu wengi sana na kusaidia kulipa thamani soko la machugwa kuzalisha ajira nyingi inayotokana na kukusanya hayo maganda na kusaidia kwenye usafi wa mazingira hapo hapo pia wawezeshe mashine ndogo kutoka hizo taasisi za kukamua na kusindika juice ya machungwa maana machungwa mengi kipindi cha msimu wake yanaoza sokoni na bei yake kushuka sana kitu kinachowaumiza wakulima wengi.
Mbali na machungwa pia tafiti zinaonesha tunaweza kutengeneza dawa, vitamini na virutumisho mbalimbali kutokana na mabaki ya maganda ya matunda mbalimbali kama vile maembe, nanasi, papai n.k haya mabaki tumekuwa tukiyatupa au mara nyingi huwa yanatumika tu kama chakula cha wanyama lakini zaidi sana tunaweza kuyaongezea thamani zaidi kupitia hizi taasisi kutengeneza mashine zakufanya uchakataji wa kuyaongezea thamani zaidi haya mabaki na kama ni ghali kumudu kununua pia wafanye mpango uleule wa kukusanya wakulima au watu kwenye kikundi alafu kuwawezesha na hizo mashine pia mafunzo jinsi ya kufanya hii itachangia ajira kwa watu wengi kuinua kipato cha mtu mmoja mmoja na pato la taifa kwa ujumla. Hii pia itasaidia kukua kwa sekta ya kilimo kupitia kuajiri watu wengi kwenye uzalishaji wa hayo matunda kutokana na soko lake kukua.
Kwahiyo ifike wakati hizo taasisi zibadilike na kubadilisha ile dhana ya kuonesha wana mashine fulani kwenye maonesho mbalimbali na kuishia hapo au kuuza kwa bei ghali uwe mpango kwa wananchi husika hizo mashine kuwafikia kwa utaratibu fulani hata kama ni kwa mkopo lakini kwa sababu watakuwa wanazalisha watakuwa na uwezo wa kurudisha kama wakibadili huo mtazamo wao basi watazalisha ajira nyingi kupitia sekta ya kilimo na ajira kwa hao watu watakao kuwa wana tumia moja kwa moja hizo mashine
Kuwe na mikakati kwa kila mkoa unaozalisha zao fulani au matunda fulani hizo teknolojia zipelekwe huko huko kuwapa mafunzo huko huko na kuwakusanya kwenye vikundi kisha kuwapa hiyo teknolojia na kuanza uzalishaji hii itasaidia wananchi wanao ishi hasa huko vijijini kuwakwamua kiuchumi na kuwawezesha kumudu gharama zao za maisha. Maana njia pekee ya kusaidia kuondoa umaskini hasa vijijini ni kuwapelekea teknolojia hukohuko.
Ukiangalia nchi zilizo endelea kama China inawasaidia wananchi wake na teknolojia moja kwa moja huko vijijini walipo kuweza kufanya kilimo cha kisasa na chenye tija zaidi kwa kuwawezesha kwenye vikundi kama ya hizo taasisi zinazolisha pembejeo mbali mbali za kilimo ni kuhakikisha hao wakilima wananufaika na hiyo teknolojia huku wakijua kwa kuwawezesha wakulima watakuwa wamezalisha ajira nyingi na kuongeza pia uzalishaji wa chakula na kuchangia pato la nchi kwa ujumla.

Upvote
0