Cute Wife
JF-Expert Member
- Nov 17, 2023
- 1,906
- 5,000
Wakuu,
Haya tuendelee na unafiki!
=====
Taasisi ya Focus on Tanzania (FOTO) imesema imeridhishwa na mchakato wote wa uchaguzi kwa namna ulivyoendesha kwa mujibu wa utafiti waliofanya na kuthibitisha kuwa uchaguzi wa serikali za mitaa kwa mwaka 2024 umekuwa wa huru na haki.
Kauli hiyo imetolewa na Mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo Ndugu Walles Mayunga ambapo ameeleza kuwa uchaguzi huu umefata kanuni na taratibu za kitaifa na kimataifa licha ya kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa baadhi ya wafuasi wa vyama vya siasa.
Kupata taarifa na matukio ya kimkoa kuhusu Uchaguzi Serikali za Mitaa ingia hapa: LGE2024 - Special Thread: Orodha ya Mijadala ya Mikoa yote Tanzania Bara inayoshiriki katika Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024
Amesisitiza kuwa katika kila uchaguzi kunakuwa na misingi, kanuni na taratibu ambazo zinaongoza uchaguzi huo na ambazo zinatakiwa kufatwa wakati wote wa mchakato wa uchaguzi.
Aidha amewataka vijana kote nchini kuacha kutumika vibaya na baadhi ya wanasiasa ambao kwa masilahi yao wanawatumia vijana kuingia barabarani na kuandamana wakipinga uchaguzi ambao umemalizika kuwa haukuwa wa huru na haki kitu ambacho amesema ni kinyume na sheria