DOKEZO Taasisi ya kukopesha ya Imarika inavyodhulumu mali za wateja kwa mikopo umiza mkoa Dodoma

DOKEZO Taasisi ya kukopesha ya Imarika inavyodhulumu mali za wateja kwa mikopo umiza mkoa Dodoma

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'

Mzee wa Code

Member
Joined
Sep 23, 2024
Posts
61
Reaction score
91
Sisi wakazi wa Dodoma tumechoshwa na mmiliki wa kampunı ya ukopeshaji Fedha ya Imarika, imekuwa ikitoa mikopo umiza kwa riba kubwa ya asilimia 40, imekuwa akidhulumu dhamana zetu kwa kubadilisha mikataba.

Mmiliki kwa kuwa tabia yake ni kudhulumu mali zetu, pindi unapotaka kumaliza deni ofisi yake inakunyima ushirikiano na pamoja inakutengezea mikataba fake, baya zaidi amekuwa na tabia ya kuvamia mali za zetu bila vibari vya mahakama au kupitia ofisi za Mitaa.

Amekuwa akivunja Sheria na haki za binaadamu yeye na walinzi wake anaowatumia kuvamia nyumba zetu kwa kutupa vitu vyetu nje huku Mamlaka za serikali zikimuangalia tu.

Mfano walipovamia nyumba yetu kwa deni la milioni 3, tuliwapigia viongozi wa mtaa, na Mkuu wa wilaya hakuna msaada wowote. Ametudhulumu Nyumba yetu iliyopo area C na dhulma hii amehalalishwa na taasisi mbalimbali za serikali kama ofisi za jiji ambapo walifanya mabadiliko ya jina la umiliki wa Nyumba yetu bila idhini ya baba yetu ambaye alikuwa mahututi kitandani.
 
Back
Top Bottom