Taasisi ya Mkapa kujenga nyumba 700 vijijini

Taasisi ya Mkapa kujenga nyumba 700 vijijini

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Joined
Feb 3, 2009
Posts
42,872
Reaction score
34,363
mkapa.jpg

Rais Mstaafu wa Awamu ya tatu,Benjamin Mkapa.

KWA UFUPI
Taasisi ya Mkapa Foundation, imekuwa ikiisaidia Serikali katika kuboresha huduma za afya kwa watu wa vijijini ambao mara nyingi wamekuwa wakikabiliwa na matatizo mbalimbali katika kupata huduma. Msaada wa taasisi hiyo kwa Serikali ni pamoja na kuipatia watumishi wa afya wanaopelekwa vijijini.


Hatua hiyo inalenga katika kuboresha mazingira ya kazi kwa watumishi wa sekta ya afya huko vijijini.

Arusha. Taasisi ya Mkapa Foundation, inatarajia kujenga nyumba 700 za watumishi wa afya wanaotoa huduma katika maeneo ya vijijini.

Hatua hiyo inalenga katika, kuwaboreshea mazingira mazuri watumishi hao ili waweze kutoa huduma kwa ufanisi.

Hayo yalibainishwa juzi na Ofisa Mipango wa Kitengo cha Uwezeshaji katika taasisi hiyo, Pamela Maro, alipokuwa akizungumzia shughuli zinazofanywa na taasisi hiyo katika kuboresha huduma za afya vijijini.

Alisema lengo la ujenzi wa nyumba hizo ni kuboresha huduma kwa wananchi wa vijijini wanaokabiliwa na changamoto nyingi.

Maro alisema taasisi hiyo imekuwa ikishirikiana na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kuhakikisha kuwa changamoto zinazowakabili wananchi wao vijijini zinatatuliwa.

Alisema mbali na kujenga nyumba hizo taasisi hiyo pia imekuwa ikiisaidia Serikali kwa kuipatia watumishi wa afya na kuwapeleka katika maeneo ya vijijini.

Alisema tayari taasisi imeshaisaidia Serikali watumishi 230 wa sekta hiyo ambao wamepelekwa katika vituo mbalimbali vya afya na hospitali za wilaya.

Ofisa huyo alisema katika kuhakikisha kuwa huduma zinaboreka zaidi, taasisi imekuwa ikitoa mafunzo mbalimbali kwa timu za wasimamizi wa afya walioko wilayani.

Maro alisema mafunzo hayo pia yametolewa kwa wasimamizi wa vituo vya afya katika mikoa mbalimbali.

Alisema pamoja na jitihada hizo, lakini tatizo la uhaba wa watumishi katika vituo na hospitali mbalimbali ni kubwa sana.http://www.mwananchi.co.tz/habari/Kitaifa/-/1597296/1726400/-/128pt9r/-/index.html
 
Shukrani kwa Mkapa Foundation. Taasisi zingine ziige mfano huu.

Tunasubiri na Kikwete foundation inayokuja sijui itajikita kwenye nini akiwa na maswahiba wake wakuu wa Homeshopping center,TSN n.k
Mwinyi yeye ameamua kuwa imam na sadaka zake kutoka kwenye mashamba yake ya miwa,hotel na majengo dar es salaam anajengea misikiti na kufuturisha
 
Back
Top Bottom