Pfizer
JF-Expert Member
- Mar 25, 2021
- 590
- 807
Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amekutana na kufaya mazungumzo na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya MO Dewji, Imran Sherali ambaye ameambatana na Mbunge wa Singida Kaskazini, Mhe. Ighondo Ramadhani na mbunge wa Viti Maalum, Mhe. Bupe Mwakang’ate jijini ofisi ndogo za Wizara ya Maji DUWASA jijini Dodoma.
Taasisi ya MO Dewji kupitia Mkurugenzi Mtendaji wake imesema ina lengo la kushirikiana na Wizara ya Maji katika utekelezaji wa miradi ya maji hasa katika uchimbaji wa visima hususani maeneo yenye changamoto ya vyanzo vya Maji kama Mkoa wa Singida pamoja na uboreshaji wa miuondombinu ya Maji.
Waziri Aweso akizungumza baada ya maelezo ya Bwana Imran, ameikaribisha Taasisi hiyo na kusema kwamba milango iko wazi ili kuweza kushirikiana na serikali ya awamu ya sita katika masuala ya maji na kueleza ni kwa namna gani Sekta ya Maji imekua ikifanya kazi kwa mashirikiano na wadau mbalimbali lengo ikiwa ni kuhakikisha mwana Mama anatuliwa ndoo kichwani.