Habari wandugu,
Hii taasisi ya ndoa naona inahitaji maboresho makubwa kuendana na wakati kwani kwa sasa mitazamo na tabia za watu zimebadirika sana.
Hivyo kubaki na taasisi yenye misingi ile ile kwa miaka na miaka si jambo sahihi. Ndio maana sasa ndoa zinavunjika, wanandoa wanasababishiana madhara.
Kwanini sasa tusikubali ndoa za mikataba kama wenzetu? Ili angalau ukiona ndoa haikizi mahitaji yako unajua kabisa baada ya mwaka mkataba utaisha na namna ya kutoka imeelezwa vyema na mlikubaliana pamoja. Kuliko hii ya sasa unaingia kwa mapenzi (na mapenzi yenyewe ndio haya upofu unakuja zinduka baadae unaona daaah kumbe sikuwa na taarifa za kutosha) na ikifika wakati wa kutoka Mume lazima apate hasara kiuchumi.
Kwanini sasa tusianze kusupport pre-nuptials?