- Source #1
- View Source #1
- Source #2
- View Source #2
Nimekutana na hii taarifa iliyotolewa na The Chanzo ikidai kuwa Padri Dkt. Kitima kupitia taasisi yake ya CK ana mradi wa kugawa bidhaa tajwa hapo juu,
Wasiwasi wangu isije kuwa wanamchafua Padri kutokana na maoni ambayo amekuwa akiyatoa katika nyanja za Siasa, Uwajibikaji na Utawala Bora.
Wasiwasi wangu isije kuwa wanamchafua Padri kutokana na maoni ambayo amekuwa akiyatoa katika nyanja za Siasa, Uwajibikaji na Utawala Bora.
- Tunachokijua
- Padre Charles Kitima ni katibu wa baraza la maaskofu katoliki Tanzania (TEC) ambaye alipata daraja takatifu ya upadre takribani miaka 27 iliyopita ambapo mwaka 2022 aliadhimisha Jubilei ya miaka 25 ya Upadre katika Parokia ya Kristu Mfalme Siuyu Jimbo Katoliki Singida mahali alipozaliwa.
Padre Kitima amekuwa ni moja kati ya viongozi wa dini ambao wamekuwa mstari wa mbele katika kutoa elimu ya kiraia ili kuwawezesha wananchi kushiriki kikamilifu kwenye michakato ya kidemokrasia, kadhalika amekuwa akikemea na kukosoa ukiukwaji wa taratibu za kidemokrasia nchini hasa katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa Novemba 27, 2024.
Kumekuwapo na taarifa inayosambaa mtandaoni ikidaiwa kutolewa na The Chanzo, ambayo inasema Taasisi ya Katibu Mkuu TEC, Padri Dkt. Charles Kitima (CK Foundation), yadaiwa kugawa bidhaa za kuchochea mabadiliko ya homoni kwa wanafunzi wa kiume shuleni.
Taarifa hiyo imehifadhiwa hapa.
Je ni upi uhalisia wa taarifa hiyo?
Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck ulibaini kuwa taarifa hiyo si ya kweli na haikutolewa na The Chanzo. Vilevile hakuna taasisi inayotajwa kuwa ya Padri Kitima (CK foundation) iliyosajiliwa nchini Tanzania hivyo taarifa kuhusu taasisi hiyo ambayo haipo juu kugawa bidhaa za kuchochea mabadiliko ya homoni kwa wanafunzi wa kiume shuleni si ya kweli.
Aidha Chapisho la taarifa hiyo linaonesha kuwa ilitolewa mnamo tarehe 11 Novemba 2024 lakini katika kurasa rasmi za mitandao ya kijamii ya The Chanzo hakukuwa na taarifa hiyo hivyo kuonesha kuwa ilitengenezwa na wapotoshaji.
Kadhalika JamiiCheck ilibaini mapungufu kadhaa katika chapisho hilo, ambayo yanadhihirisha utofauti dhidi ya taarifa ambazo hutolewa na The Chanzo. Moja ya mapungufu hayo ni kutofautiana kwa mwandiko (fonts) unaotumika kuandika kichwa cha habari (Title) ambapo haufanani na ule unaotumiwa na The Chanzo, kutofautiana kwa ukubwa wa mstari unaotenganisha sehemu ya chini ya maandishi na juu yenye picha ambapo katika chapisho linalopotosha lina mstari mwembamba ukilinganisha na machapisho rasmi ya The Chanzo.
Aidha katika kutafuta uhalisia zaidi wa jambo hilo JamiiCheck imewasiliana na Uongozi wa The Chanzo ambapo wamekana wamekanusha kuhusika na taarifa hiyo na kusisitiza kuwa taarifa zao hupatikana kwenye kurasa rasmi za mitandao ya kijamii.
“Kumekuwapo na taarifa potofu zikitumia mfanano wa alama zetu, kama hii taarifa ambayo si ya kweli, taarifa zetu zote rasmi zinapatikana katika majukwaa yetu rasmi ya The Chanzo.” umesema uongozi wa The Chanzo.
HIi si mara ya kwanza kwa The Chanzo kutengenezewa taarifa za uzushi ambapo Septemba 12, 2024 JamiiCheck ilikanusha pia taasisi hiyo kuhusika kuchapisha taarifa iliyodai Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe alimshukuru Rais Samia kwa kuungana nao kuomboleza msiba wa kada na kiongozi wao Ali Kibao.