JamiiForums
JF Official Account
- Nov 9, 2006
- 6,229
- 5,285
Taasisi Ya Rockwool Kutoka Denmark Na Recoda Yazindua Ubunifu Mpya Wa Kupeleka Maendeleo Vijijini Tanzania
Jumatatu 11[SUP]th[/SUP] Machi mkutano mkubwa utafanyika Dar es Salaam wenyeji wakiwa ni taasisi ya Denmark ya Rockwool na Ubalozi wa Denmark Tanzania. Katika mkutano wa waandishi wa habari ubunifu mpya wa maendeleo vijijini miongoni mwa wakulima wadogo wadogo unazinduliwa pamoja na ujuzi wa matokeo yaliyotoka na kubadilika kwa hali ya maisha ya wakulima washiriki wa mradi amabyo imechapishwa katika kitabu cha chaguo la mkulima Farmers choice).
Tangu 2006, ubunifu wenye uwezo wa kuleta mabadiliko katika usambaaji wa teknolojia ya kilimo umetekelezwa Kaskazini mwa Tanzania, wenye kuweka msukumo utumiaji wa mashamba darasa na kutoa kapu la uchaguzi wa teknolojia, ambalo wakulima wanaweza kuchagua ambacho kitawahudumia kwa ubora zaidi kiuzalishaji kutokana na raslimali na uwezo walio nao. Lengo/msisitizo ni kuwezesha kusambaa kwa tecknolojia bora za kilimo zenye gharama nafuu na zinazoweza kuchukuliwa na kutumika kulingana na hali halisi ya vijiji husika.
Ubunifu huu mpya wa maendeleo vijijini unajulikana kama RIPAT (Rural Initiatives for Participatory Agricultural Transformation) ukiwa na maana ya Ubunifu Shirikishi wa Mapinduzi (mabadiliko) ya Kilimo Vijijini. RIPAT inatekelezwa na shirika lisilo la kiserikali Tanzania linaloitwa RECODA, na utelezaji umewezeshwa kwa ufadhili wa fedha na mchango wa ujuzi kutoka taasisi ya Rockwool.
Kwa nyongeza katika chapisho la kitabu cha chaguo la mkulima, mwongozo (Manual) umechapishwa unaoelezea hatua kwa hatua jinsi ya kutekeleza mradi kwa mfumo wa RIAT ili kupata matokeo yaliyo mazuri; kwa hiyo wizara ya kilimo Tanzania na wadau wengine kote Tanzania, na kwa ujumla zaidi, kusini mwa Afrika wana fursa ya kupanga na kutekeleza miradi ya kilimo kwa mfumo wa RIPAT.
Mchanganuo wa takwimu za utafiti uliofanyika kwa kuhoji kaya za wakulima 2500 unaonyesha kwamba, kwa wastani, kaya ambazo zimeshiriki katika mradi wa RIPAT ukilinganisha na ambazo hazikushiriki ni kwamba
Mwanzo ilichukua muda kuona mafanikio kutokana na mazao mapya na mbinu mpya, lakini sasa tuna maisha bora, anaeleza.
Familia yake polepole imekuwa na uhakika wa chakula zaidi na kumwezesha Warimbora kuuza zaidi bidhaa za kilimo, mapato kuongezeka na hata kuwa na fursa ya kuweka akiba ya fedha katika sanduku la kikundi la kuweka akiba (VICOBA).
Warimbora ni miongoni mwa wakulima zaidi ya 2500 ambao wamefaidika kutokana na RIPAT, ambao sasa umetekelezwa kwa mfulilizo wa miradi minne ya majaribio katika wilaya tatu za kaskazini mwa Tanzania, ambazo ni Arumeru, Karatu and Korogwe, ambapo kila mradi hutekelezwa kwa muda wa miaka mitatu hadi minne. Mradi wa aina ya RIPAT unalenga vijiji nane; vikundi viwili kuanzishwa katika kila kijiji, kila kikundi kinakuwa na wakulima wadogo wadogo 30-35.
Aliyekuea mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mh. Isidore Leka Shirima aliyefuatilia kwa maakini utekelezaji wa RIAT wakati akiwa madarakani alikuwa na haya ya kusema; Nimeona kilimo cha kisasa inachotekelezwa na RIPAT kinatoa mazao mengi, na nimewasikia wakulima wakishuhudia kuongeza kwa kipato kumewawezesha kueleka watoto wao shule na hata kuwawezesha kujenga nyumba. Naiamini RIPAT Nimeiona ikifanya kazi.
Wajibu wa taasisi ya Rockwool ni kutengeneza mfumo mpya wa maendeleo vijijini miongoni mwa wakulima wadogo wadogo kuanzia Kaskazini mwa Tanzania unaotokana na shauku ya kuleta suluhisho la changamoto za kichumi na jamii zinazokabili maskini na matajiri. Kukiwa na fikira kwamba maendeleo ya kilimo Afrika ni vigumu na mara zote hushindwa, taasi ya Rockwool na RECODA wamefanya kazi kutafuta suluhisho na mfumo/mtindo mzuri wa jinsi ya kushughulikia hii changamoto; mfumo ambao unawezesha wakulima wadogo wadogo kujimudu wenyewe na kuzalisha uchumi unaokua (wenye tija).
WEBSITE: Read more about RIPAT on RIPAT: Home
TWITTER: For mentioning and debate on Twitter
we encourage the use of the hashtag #RIPATTZ

- zile zilizoshiriki zina utofauti zaidi kwa; kulima mazao bora au wanazalisha mifugo bora iliyotolewa katika kapu la uchaguzi;
- Ulimaji wa migomba ya kisasa imechukuliwa na asilimia 60 ya wakulima wa RIPAT likiwa ni zao lililopendwa zaidi kutoka katika kapu la uchaguzi;
- kuwa na uhakika wa chakula katika msimu ambao si wa uzalishaji, ambapo wakulima wa RIPAT ni chini ya asilimia 25 wanaoweza kupatwa na njaa;
- Kuwa na watoto wenye afya bora zaidi kwa asilimia 27% zaidi katika ulinganisho wa wale watoto walio chni ya umri wa miaka mitano.
- kula nyama na mayai kila wiki;